MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amemaliza mgogoro uliodumu kwa takriban miaka 15 katika eneo la kariakoo ukihusisha familia ya marehemu Abdallah Sultani Mtambo akiwemo aliekuwa mkewe Bi Malaya Mtambo na Salim Selemani Salim ambae alinunua nyumba hiyo namba 12 kiwanja namba 15 kupitia mnada wa mahakama ambapo amemkabidhi Salim Selemani Salim kama mmiliki halali alieinunua nyumba hiyo kihalali
Akizungumza leo Feb 17 Jijini Dar es salaam mara baada ya kusikiliza taarifa ya kamati aliyoiunda alipotembelea nyumba hiyo mwezi januari mwaka huu RC Chalamila amesema amejiridhisha kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya mahakama nyumba hiyo ni ya Salim Selemani Salim kwani aliinunua kisheria chini ya usimamizi wa mahakama kwa kiasi cha shilingi milioni 250 tangu mwaka 2011
Aidha RC Chalamila amesema baada ya nyumba hiyo kuuzwa kisheria baadhi ya warithi walipokea fedha hizo kutoka kwa dalali wa mahakama lakini baadhi ya warithi akiwemo Bi Malaya waligoma kuchukua fedha hiyo ambapo kiasi cha shilingi milioni 64 na laki tano ambayo hadi sasa ipo kwa dalali huyo hivyo ameelekeza dalali huyo kizikabidhi fedha hizo ziende mahakamani ali zikabidhiwe kwa wahusika kwa kuzingatia taratibu za kimahakama.
Akitoa taarifa ya kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Fabiola Mwingira amesema kamati imefuatilia kwa kina mgogoro huo na kubaini kuwa taratinu zote za kimahakama zilifuatwa baada ya warithi kutoelewana na mahakama kusimamia uuzwaji wa nyumba hiyo



.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...