Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka walimu na wadau wengine wa elimu Mkoani humo kutafsiri vema maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri kwenye masomo yao na baadae wanapohitimu masomo ili kuwa na kizazi chenye tija.



Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na wadau wa elimu katika Mkoa huo wakiwemo walimu Mkuu na maafisa wengine katika sekta hiyo RC Chalamila amesema matarajio na maono ya Serikali kwenye sekta ya elimu ni makubwa na ndio maana imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwekeza katika maeneo mbalimbali, hivyo ni muhimu kwa walimu na wadau wengine wa elimu kutafsiri maono hayo kwa vitendo.


Aidha RC Chalamila amewataka wakurugenzi, maafisa elimu na wakuu wa idara ya elimu kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zimazowakabili walimu ili kuweza kutimiza malendo na maono ya Rais Dkt Samia kwenye sekta ya elimu



Kwa upande wa Afisa elimu Mkoa wa Dar es salaam Bw Gift  Kyando  na Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw Elihuruma Maberya wameeleza hali halisi  ya elimu katika Mkoa na mipango ya kuboresha elimu huku wakizungumzia pia mkakati wa kutengeneza mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia wanafunzi watakaomaliza darasa la saba na la sita mwakani ambao wote watakwenda kidato cha kwanza mwaka 2028




Sanjari na hilo baadhi ya walimu walioshiriki mkutano huo wameiomba Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya shule ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi hususani kwenye miundombinu na madawati.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...