Wananchi wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita sasa wanaweza kupumua kwa amani baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kukamilisha ahadi yake ya kuimarisha huduma za uokoaji na zimamoto wilayani humo.

Katika hafla iliyopambwa na matumaini makubwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, amekabidhi magari ya msaada wa zimamoto ambayo yatakuwa mkombozi mkubwa katika kukabiliana na majanga ya moto na ajali za barabarani.

Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa gari hilo si kwa ajili ya kuzima moto tu, bali lina uwezo wa:

Kukata vyuma kwa urahisi,Hii itasaidia sana kuokoa watu walionaswa kwenye magari baada ya ajali,.Kubeba maji lita 400 Pamoja na foam compound lita 40 maalum kwa ajili ya kuzima moto wa mafuta (flammable liquids).

Sambamba na gari la zimamoto, Bukombe imepokea gari la kubebea wagonjwa (Ambulance). Gari hili limetengwa maalum kwa ajili ya kuwahi eneo la tukio pindi ajali zinapotokea ili kuokoa maisha ya wananchi kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Kenneth Mwakasitu, amewataka wakazi wa Bukombe kuwa na utamaduni wa kuheshimu king’ora.

"Natoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria za barabarani na kupisha gari hili linapokuwa katika dharura. Hii itatuwezesha kufanya kazi yetu kwa ufanisi na kuokoa maisha kwa wakati," alisema Mwakasitu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskasi Muragiri, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ahadi hiyo muhimu. Ameeleza kuwa ujio wa vifaa hivi unamaliza kipindi cha hofu na wasiwasi miongoni mwa wana-Bukombe pindi majanga yanapotokea.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...