Na Mwandishi wetu - Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, amesrma matokeo ya tafiti ni muhimu kwa taifa kwa kuwa yataisaidia Serikali na Wizara husika kupata suluhisho la changamoto mbalimbali, ikiwemo uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Prof Mushi ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa maendeleo ya utafiti chini ya Programu ya Utafiti wa Mabadiliko ya Tabianchi, ambapo mesema kuwa wajibu wa watafiti na wadau wa Sekta ya sayansi haupaswi kuishia katika mikutano na machapisho pekee, bali wanapaswa kufuatilia kwa karibu kuhakikisha matokeo ya tafiti yanatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.
“Hatupaswi kuishia kwenye huu mkutano pekee, bali tuwajibike kwa wananchi kwa kuwapatia matokeo ya tafiti na kuelekeza matumizi bora ya matokeo hayo,"
Ameongeza kuwa matokeo ya tafiti ni muhimu kwa taifa kwa kuwa yataisaidia serikali na wizara husika kupata suluhisho la changamoto mbalimbali, ikiwemo uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema matarajio ya Serikali kwa watafiti waliopata fedha hizo ni makubwa, na kwamba anatarajia miradi 34 kati ya hiyo kuwasilisha matokeo ya tafiti zao katika mkutano huo.
Amesema utekelezaji wa programu hiyo unahusisha vyuo vikuu na taasisi za utafiti 20 nchini, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa serikali unaolenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali.
Prof. Mushi amesema Kuwa hadi sasa programu hiyo imepatiwa jumla ya Sh bilioni 14.5, ambapo Sh bilioni 12.1 tayari zimewekezwa katika miradi 39 ya utafiti inayojikita kuchunguza na kutafuta suluhisho la changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kilimo, maliasili, afya, nishati, maji pamoja na mifumo ya kijamii na kiuchumi.
“Nitoe wito kwa watekelezaji wa miradi yote 39 kuhakikisha kila shilingi inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. COSTECH ihakikishe inasimamia vyema fedha za utafiti na kuratibu uwasilishaji wa matokeo kwa wadau wote,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt Amos Nungu, alisema kuwa hadi sasa programu hiyo imeshirikisha taasisi 13, vyuo vikuu 12 na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), huku jumla ya watafiti 200 na wanafunzi 90 wakishiriki.
Dkt Nungu aliwashukuru wafadhili wa programu hiyo, akiwataja kuwa ni SIDA na Serikali ya Norway, kwa ushirikiano wao mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa programu ya utafiti wa mabadiliko ya tabianchi nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Makamishna COSTECH Profesa John Kandoro alisema mkutano huo utakuwa na majawabu yenye ushahidi wa kisayansi ambayo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake mwakilishi wa SIDA DK Johanna Variandek alisema wataendea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tafifi mbalimbali zinafanya vizuri.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...