Na Mwandishi wetu- Dodom.
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema Wizara imekamilisha taratibu za kuanza upanuzi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam wenye lengo la kujenga magati 10 pamoja na matenki 15 ya mafuta.
Ujenzi wa magati mawili (2) ya awali yenye urefu wa mita 500 utaanza mwezi Juni, 2026 na huku ujenzi wa matenki ukiendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Prof Mbarawa ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma kwenye Mkutano na Waandishi wa habari akieleza utekelezaji wa siku 100 za Serikali ya awamu ya sita kipindi Cha pili.
"Uboreshaji huu utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena hadi tani milioni 50 kwa mwaka ndani ya kipindi kifupi, kutoka takribani tani milioni 32 za sasa"
Amesema kuanza kwa maandalizi ya ujenzi wa Bandari kubwa na ya kisasa ya Bagamoyo, Awamu ya Kwanza ya mradi huo itahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa kilometa 1.32 kwa ajili ya kuhudumia meli kubwa za kisasa (Mega Max).
Bandari hiyo ni ya kimkakati katika kupunguza msongamano wa Bandari ya Dar es Salaam na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji wa baharini katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidh Prof Mbarawa amesema katika hatua nyingine za kuendeleza huduma za bandari nchini, Serikali imeanza utekelezaji wa Mradi wa Kurasini Logistics Terminal, unaolenga kupunguza msongamano wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam na kuongeza miundombinu muhimu ya kuhudumia shehena inayoharibika haraka (perishables).
Hat hivyo Prof Mbarawa amesema Mradi huo unahusisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuhifadhi makasha kwa muda katika eneo la mita za mraba 210,000, chenye uwezo wa kuhifadhi hadi makasha 700,000.
Aidha Prof Mbarawa ameelez kuwa kwa sasa, Awamu ya Kwanza ya ujenzi katika eneo la mita za mraba 81,000 inaendelea;
Wizara imekamilisha maboresho ya Bandari za Kemondo na Bukoba katika Ziwa Victoria na bandari hizi zinatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji kati ya Bukoba, Mwanza na bandari za Uganda.
"Hatua hii itaongeza biashara ya kikanda na kupunguza gharama za usafiri kwa njia ya maji;
Katika hatua nyingine, Serikali kupitia TPA inaendelea na ujenzi wa bandari ya Kisiwa Mgao Mtwara mradi ambao ni maalum kwa ajili ya kuhudumia shehena ya mzigo mchafu (Dirty Cargo) kama vile Makaa ya Mawe na Saruji. Kwa sasa, Mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa mradi huu ambao hadi sasa umefikia asilimia 18 ya utekelezaji"
Hata hivyo amesema mukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi katika utendaji wa Bandari ya Mtwara na vile vile uimarishaji na utunzaji wa mizigo katika Ziwa Nyasa, Serikali kupitia TPA inaendelea kutekekeza mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay unaohusisha ujenzi wa gati ya kuhudumia shehena ya magari (RO-RO) na meli, jengo la Utawala, Uzio, Barabara, Jengo la Kuhifadhia Mizigo pamoja na Jengo la Abiria. Mradi huu kwa sasa umefikia asilimia 46 ya utekelezaji wake.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...