Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuimarisha elimu jumuishi kwa kuchapa na kusambaza vitabu pamoja na maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya wanafunzi wasioona na wenye uono hafifu katika shule za msingi na sekondari nchini.
Hatua hiyo imeambatana na kuondoa vikwazo vya kimuundo na kimfumo kupitia mwongozo maalumu ulioandaliwa, unaoweka viwango vya ubora na kubainisha majukumu ya wadau mbalimbali, kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanapata elimu yenye ubora na usawa.
Akizungumza leo Februari 6, 2026 jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, wakati wa ufunguzi wa kikao cha wawakilishi wa walimu wanawake na walimu wenye ulemavu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, amesema serikali pia inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wakiwemo walimu wenye ulemavu, ununuzi wa vitendea kazi, pamoja na utoaji wa elimu kuhusu mwongozo wa utoaji wa huduma kwa watumishi.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, serikali imenunua na kusambaza vifaa maalumu vya kielimu na kisaidizi vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.5, ambapo jumla ya walimu wenye ulemavu 1,055 wamenufaika na vifaa hivyo.
Amewaasa walimu wote nchini, wakiwemo wanawake na walimu wenye ulemavu, kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kutekeleza kwa vitendo Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Suleiman Komba, ameomba serikali kupitia Wizara ya Elimu kusaidia uwepo wa malipo ya muda wa ziada (overtime) kwa walimu, akieleza kuwa kisheria muda wa kazi ni masaa nane, lakini walimu hulazimika kufika shuleni mapema kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi, amesema walimu wataendelea kuwa kioo na walezi wa jamii.
Awali, akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mwakilishi wa Walimu Wanawake CWT, Elizabeth Welema, ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza siku za likizo ya uzazi kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti, pamoja na juhudi zinazofanywa kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu bila ubaguzi.
Hatua za Serikali ya Awamu ya Sita zinaonesha dhamira ya kuimarisha elimu jumuishi na kuboresha mazingira ya walimu, wakiwemo wanawake na wenye ulemavu, ushirikiano kati ya serikali na CWT unaendelea kuwa muhimu katika kufikia elimu bora, yenye usawa na kutimiza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...