Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha

ONGEZEKO la vitendo vya ukatili na uhalifu vinavyoendelea nchini ni matokeo ya ukosefu wa mfumo wa malezi na makuzi bora ya watoto tangu wakiwa wadogo, wakati Mama akiwa mjamzito na baada ya kuzaliwa.

Hayo yameelezwa leo 6 Februari 2026 na Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha, Denis Mgiye alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kuhusu mpango wa makuzi na malezi kwa baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha yanayoendelea katika mji wa Karatu.

Migiye ambaye pia ni mratibu wa mpango wa malezi na makuzi ya mtoto Mkoa wa Arusha, amesema mtoto tangu akiwa mimba na baada ya kuzaliwa anapaswa kupewa malezi bora ya Baba na Mama Ili kumkuza katika hali bora na kumjenga kiakili, kimaadili, afya, elimu na usalama.

“ Watoto wengi wanaharibika wakiwa bado wadogo baada ya kukosa malezi bora akiwa katika hatua za makuzi, mtoto anatakiwa kusemeshwa tangu akiwa mimba na hata baada ya kuzaliwa,” amesema.

Amesema takwimu zinaonyesha kuwa watoto wenye umri wa miaka 4 na 5 ukuaji wao umekuwa kwa asilimia 65 jambo ambalo linarudisha nyuma mfumo mzima wa maisha ya mtoto.

Afisa kutoka taasisi ya SOS ambao ndio wafadhili wakuu wa mafunzo hayo,Husna Selungwi  amesema wamekutanisha waandishi kupitia program ya Arusha Innovation Ili kusaidia kusambaza elimu ya makuzi na malezi kwa jamii.

Amesema katika Mkoa wa Arusha na maeneo mengine nchini watu wengi wamekuwa hawana elimu ya makuzi na ndio sababu mtoto akikua matatizo mengi yanakuwa yanaibuka ikiwemo kufeli kielimu.

“ umri wa awali wa watoto kwenda elimu ya awali imekuwa ni ndogo tofauti na miongozo ya kitaifa inavyoelekeza, hili linajitokeza Kwa sababu wazazi hawana elimu ya makuzi na malezi, tumeita waandishi wa habari kuwapa elimu hii Ili tusaidiane kutoa elimu zaidi Kwa jamii kupitia kalamu zenu,” amesema na kuongeza:

“ Tunahitaji nguvu kubwa zaidi kutoa elimu ndio sababu tunatumia vyombo vya habari kuendeleza kusisitiza umuhimu wa malezi Bora Kwa watoto,” amesema.

Awali akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu amewataka waandishi wanaoshiriki mafunzo hayo kuyazingatia Ili kujenga jamii Bora na sikivu.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi wa habari kwa kuwa na wao  pia ni walezi, na hivyo kuwataka kutumia mafunzo hayo kama fursa.

“ Tumepata nafasi hii tuitumie kama fursa, na kuacha kufanya mambo kwa mazoea, kwa Sasa taaluma yetu umebanwa sana, tukipata fursa kama hizi ndio tunapaswa kuzitumia kujijenga na kuigeuza kuwa sehemu ya kupata kipato, ukiwa unaandika habari za watoto na wewe utaonekana huko duniani hiyo ni fursa,” amesema.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...