Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imeandika historia nyingine baada ya kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo Tuzo ya Utoaji Huduma Bora kwa Wateja (Customer Service Excellence Award), inayotolewa na Wizara ya Maji kwa mamlaka za maji zinazoonesha viwango vya juu vya ubora wa huduma nchini.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika Februari 23, 2026, Jijini Arusha, ikiwakutanisha wataalamu wa sekta ya maji pamoja na wawakilishi wa mamlaka mbalimbali za maji kutoka mikoa tofauti ya Tanzania.

Katika ushindani huo, SOUWASA imeibuka kinara katika kundi la Mamlaka Kubwa za Maji zenye zaidi ya wateja 20,000, ikishinda kutokana na maboresho makubwa ya mifumo ya huduma kwa wateja, upokeaji na utatuzi wa malalamiko kwa wakati, pamoja na kuimarisha mawasiliano kati ya mamlaka na wananchi.

Tuzo hiyo imekabidhiwa rasmi na Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso (Mb), ambaye aliipongeza SOUWASA kwa ubunifu na juhudi zinazoendelea katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa viwango vinavyokidhi matarajio.

Ushindi huo unaendelea kuiweka SOUWASA katika ramani ya ubora wa huduma nchini, na kuwa mfano wa kuigwa kwa mamlaka nyingine za maji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa wakati na kwa viwango stahiki



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...