Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia wamesaini Hati ya Makubaliano kuhusu masuala ya kiuhamiaji.

Hati hiyo ya Makubaliano imelenga kuondoleana hitaji la visa kwa Pasipoti za kidiplomasia na za kiutumishi pamoja na mashirikiano katika masuala ya uhamiaji baina ya nchi hizo mbili.

Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Serikali ya Somalia,Jenerali Abdullahi Sheikh Ismail Fartaag.

Akizungumza baada ya kusaini Hati ya Makubaliano , Waziri Katambi ametambua ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo pamoja na mashirikiano yaliyopo katika masuala ya usalama wa raia na kuhamisha wafungwa.

Vilevile Waziri Katambi ameeleza kuwa  Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchi zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha usalama na Amani vinatawala katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tukio hilo pia limehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Ayoub Mohamed Mahmoud na Katibu Mkuu,Ally Senga Gugu.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...