Baadhi ya Matukio katika Picha kwenye Ujenzi wa Bandari Kavu Kurasini jijini Dar es Salaam.




Mkurugenzi Mkuu wa TASAC akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa Bandari Kavu Kurasini Jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kusababisha msongamano bandarini hapo na kufanya Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kujenga bandari kavu ili kupunguza msongamano na kuongeza kasi ya huduma.

Salum ameyasena hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kurasini unaotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambapo Mradi huo unalenga kuongeza ufanisi wa kuhudumia makasha katika Bandari ya Dar es Salaam, ambayo kwa sasa inapokea shehena kubwa kutokana na maboresho ya miundombinu na mchango wa sekta binafsi katika kuhudumia meli.

“ASAC tumekuja kutoa maoni ya namna ya kuboresha ujenzi wa bandari hii na pia kujipanga kwa ajili ya kufanya ukaguzi na mradi huu ukikamilika unaweza kuhudumia zaidi ya makasha 700,000, jambo ambalo ni faida kiuchumi na kuleta mageuzi katika uwezo wa bandari yetu"amesema Mkurugenzi Mkuu Salum

Aidha ameitaka TPA kujipanga kupeleka wadau wengine ili waweze kuona mradi huo ili nao watoe maoni yao.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus, ameishukuru TASAC kwa kutembelea mradi huo wa Kurasini “Logistic Park”. Wkati akizungumza amebainisha kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 220,000 limekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na litakapokamilika litaongeza ufanisi wa kupokea na kuhifadhi mizigo kwa kiwango kikubwa.

“Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikifanya vizuri, ambapo kwa miezi ya hivi karibuni imehudumia zaidi ya tani milioni 16 za mizigo.Mradi wa Kurasini unatarajiwa kukamilika Aprili 2026 na utakapokamilika utaongeza uwezo wa kupokea makontena mara mbili, kuongeza kasi ya meli kupakia na kuondoka, na kuvutia meli nyingi zaidi kutia nanga bandarini”, amesema Bwana Gallus.

Mradi huu utakapokamilika utakuwa umeuganishwa moja kwa moja na barabara, reli ya SGR na MGR, sambamba na uwepo wa taasisi mbalimbali za serikali zinazotoa huduma bandarini ili kuharakisha utoaji huduma hapo bandarini. Ujenzi mradi huu unafanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Aprili 2026 na kuanza kutoa huduma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...