Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kaskazini, Arusha limeteketeza tani tatu za bidhaa zisizo salama katika dampo la jiji la Arusha mapema leo.

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na vyakula ambavyo havijasajiliwa, vipodozi vyenye viambata hatarishi kwa afya, bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi (expired) pamoja na nguo za ndani za mitumba.

Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati endelevu ya TBS ya kulinda afya na usalama wa wananchi kwa kuondoa sokoni bidhaa zisizokidhi viwango vilivyowekwa.

Aidha, hatua hiyo inalenga kujenga imani ya walaji juu ya ubora wa bidhaa zinazopatikana sokoni na kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa salama, lenye ushindani na mchango chanya katika maendeleo ya taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...