Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kaskazini limeteketeza jumla ya tani 45 za bidhaa za vyakula zilizokwisha muda wake wa matumizi katika dampo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati endelevu ya TBS ya kulinda afya na usalama wa wananchi kwa kuondoa sokoni bidhaa zisizo na viwango.

Aidha, inalenga kujenga imani ya watumiaji kwa ubora wa bidhaa zinazopatikana sokoni na kuhakikisha soko linakuwa salama.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa udhibiti ubora Mwandamizi kwa niaba ya Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini, Bw. Edward Mwamilawa, alisema operesheni za ukaguzi zinaendeleakufanyika mara kwa mara katika maduka na maghala.

“Tutaendelea na ukaguzi na kuondoa sokoni bidhaa zisizokidhi viwango alisema Bw. Mwamilawa.

Aliwataka wananchi kuwa makini wanaponunua au kuagiza bidhaa kwa kuzingatia tarehe za mwisho wa matumizi, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa umma katika kubaini na kuripoti bidhaa hatarishi.

Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Bi. Sauda Leveri, alisema ukaguzi utaendelea sambamba na uthibitishaji wa vibali vya TBS katika maeneo ya biashara.

“Wananchi wanapaswa kuwa waangalifu wanapotumia bidhaa, hasa za vyakula, ili kuepuka madhara ya kiafya,” alisema Bi. Leveri.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...