Na Pamela Mollel, Arusha
Wanahabari wametakiwa kutumia kalamu zao kulinda mazingira na kutetea haki za jamii kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya uharibifu wa mazingira nchini na duniani kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanahabari ya Kusaidia Jamii za Asili (MAIPAC) wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi wa mazingira kwa wanahabari wa Kanda ya Kaskazini na Kati.
Mafunzo hayo yameanza leo Februari 5, 2026 jijini Arusha yakiwashirikisha wanahabari 35 kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Singida na Dodoma, yakidhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji wa THRDC, Wakili Halima Sonda, amesema wanahabari wana jukumu muhimu la kuhabarisha umma kuhusu athari za uharibifu wa mazingira ikiwemo uchafuzi, ukataji miti na uchimbaji holela wa madini.
Amesema kupitia mafunzo hayo, wanakusudia kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuandika habari za kina zitakazosaidia kuelimisha jamii na kuchochea hatua za uhifadhi wa mazingira.
Naye Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma, amesema uandishi wa habari za mazingira una mchango mkubwa katika kulinda haki za binadamu, hususan kwa jamii za asili zinazotegemea rasilimali za mazingira kuendesha maisha yao.
Ameeleza kuwa taasisi hizo mbili zinatarajia kuwafikia wanahabari 140 nchi nzima kupitia mafunzo hayo yatakayogusa pia masuala ya mabadiliko ya tabianchi, udhibiti wa taka ngumu, uhifadhi wa wanyamapori pamoja na matumizi endelevu ya ardhi.
Kwa upande wake, Wakili Paulo Kisabo aliyetoa mada kuhusu sheria za ardhi, mazingira na habari, amesisitiza wanahabari kuzingatia misingi ya kisheria wanapotekeleza majukumu yao, akibainisha kuwa sheria nyingi zinawalinda wanahabari wanapotimiza wajibu wao kwa weledi.
Mafunzo hayo yanaendelea jijini Arusha, huku yakitarajiwa kuendelea katika kanda nyingine nchini kwa lengo la kuongeza idadi ya wanahabari wenye ujuzi wa kuandika na kuchunguza masuala ya mazingira.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...