NA DIANA DEUS_BUKOBA.
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TIZESA) imewaahidi wawekezaji wazawa kuanzisha madawati ya uwekezaji katika kila halmashauri, yatakayounganisha taasisi zote zinazohusika na usajili wa masuala ya uwekezaji ili huduma zote zipatikane katika dawati moja na kurahisisha hatua za kuanza uwekezaji.
Taasisi ya TIZESA inaendelea na kampeni maalum ya kuhamasisha uwekezaji kwa lengo la kusogeza huduma za uwekezaji hadi ngazi ya mikoa na halmashauri, na kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa.
Akizungumza katika kongamano la wadau wa uwekezaji wa ndani mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Bodi ya TIZESA, Balozi Azizi Mlima, amesema taasisi hiyo imelenga kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi ili kuwawezesha kupata unafuu wa mitaji, pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria na taratibu za uwekezaji, ikiwemo kuwapunguzia adha wawekezaji kwa kuweka dawati moja la kupata huduma zote.
Ameeleza kuwa licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa uwekezaji kwa baadhi ya Watanzania, elimu na mipango ya TIZESA imeanza kuzaa matunda kwa kuwahamasisha wananchi kuwekeza zaidi ndani ya nchi, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kukuza uzalishaji wa ndani.
Amesema TIZESA inaangazia fursa mbalimbali katika Kanda ya Ziwa, ikiwemo mkoa wa Kagera ambako kuna fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo kilimo cha mazao ya biashara kama maparachichi, ufugaji wa kisasa, ufugaji wa samaki na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo.
Aidha, wananchi wamekumbushwa umuhimu wa kumiliki hati za nyumba na viwanja kama nyenzo muhimu ya kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuanzisha au kupanua miradi ya uwekezaji.
Wawekezaji walioshiriki kongamano hilo wamepongeza hatua za TIZESA kuona umuhimu wa kufikisha elimu na kuweka mpango wa kufungua madawati ya uwekezaji katika ngazi ya halmashauri, wakieleza kuwa ni hatua muhimu ya kutambua changamoto zao katika uwekezaji na kurahisisha hatua za kujisajili katika uwekezaji.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...