BAADA ya kusimama kwa muda kufuatia mchakato wa maboresho ya kiufundi na kiuendeshaji, huduma ya kidijitali ya usafiri na usafirishaji wa mizigo ya Swifpack, inayomilikiwa na Shirika la Posta Tanzania -TPC, imerejea rasmi, ikiwa na mabadiliko yanayolenga kuimarisha utoaji wa huduma na kukabiliana na mahitaji ya sasa ya watumiaji katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Huduma hiyo imefanyiwa maboresho yanayolenga kuongeza ufanisi wa mfumo, kuimarisha usalama na kurahisisha matumizi kwa abiria, madereva na wafanyabiashara ambapo maboresho hayo yamezingatia changamoto zilizojitokeza hapo awali pamoja na maoni ya watumiaji wa huduma hiyo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam kuhusu kurejea kwa Swifpack, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania, Ferdinand Kabyemela, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Shirika hilo kuhakikisha linatoa huduma za kidijitali zinazoendana na mahitaji ya soko na mabadiliko ya teknolojia.

Ameeleza kwamba mfumo wa Swifpack umeimarishwa katika mawasiliano kati ya dereva na mteja pamoja na eneo la malipo, hatua inayolenga kuongeza uwazi na kupunguza changamoto za uendeshaji wa safari na usafirishaji wa mizigo.

Aidha ujuo wa huduma hiyo umeweka mkazo kwenye ustawi wa madereva kwa kuweka makato madogo ya uendeshaji wa mfumo, pamoja na kutoa fursa za bima ya afya, kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na mpango wa umiliki wa simu janja kwa utaratibu nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...