Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua dawati maalum la uwezeshaji biashara za Forodha kwa wafanyabiashara wa Kariakoo pekee ili kuharakisha upatikanaji wa huduma za kiforodha kwa wafanyabiashara hao.
Akizindua Dawati hilo Februari 10.2026 jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema uzinduzi wa dawati hilo ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua soko la Kariakoo Februari 08.2026 la kutaka kuwekwa kwa mazingira rahisi ya kufanya biashara.
Amesema lengo la dawati hilo ni kuwezesha na kurahisisha biashara za wafanyabiashara wa Kariakoo ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa urahisi na kwa wakati ikizingatiwa kuwa soko hilo linatoa huduma kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema dawati hilo maalum litafanya kazi saa 24 na kuwa wanafanya utaratibu wa Bandari kavu nazo zifanye kazi saa 24 na shughuli zitakazofanyika ni kupokea mizigo, kuikagua na kuitoa mapema baada ya taratibu wa ukaguzi kukamilika.
"Niwahakikishie wafanyabiashara wote kuwa TRA imejipanga kuendelea kutenda haki kwa walipakodi wote na kutoa huduma kwa usawa ili kuleta usawa sokoni" amesema Kamishna Mkuu Mwenda.
Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa Bw. Juma Bakari Hassan amesema dawati hilo litaongeza kasi ya utoaji huduma kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ambao asilimia kubwa ya mizigo yao inatumia Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wao baadhi ya Walipakodi waliokwenda kupatiwa huduma akiwemo Nafsa Momba, Hassan Juma na Richard Haule wamepongeza kuanzishwa kwa dawati hilo ambalo litawqrahisishia kupata huduma za forodha kwa kuwatatulia changamoto ambazo huwa zinajitokeza wakati wa kutoa mizigo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...