Na Pamela Mollel,Arusha
Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) imepongezwa kwa jitihada zake za kipekee katika usimamizi wa vyama vya ushirika, huku balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi, akisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika uendeshaji wa shughuli za ushirika.
Pongezi hizo zimetolewa wakati Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, akitoa maelezo ya kina kuhusu mfumo wa kisasa wa usimamizi wa vyama vya ushirika katika banda la maonyesho, wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Jijini Arusha. Dkt. Ndiege alisisitiza jinsi TCDC inavyotumia mfumo huu wa kidijitali kusimamia vyama vya ushirika kwa ufanisi, kuimarisha uwazi, na kuongeza uwajibikaji wa taasisi hizo.
Akifungua Kikao cha Sita cha Serikali Mtandao (e-GA) kinachoratibiwa na Wizara ya Kilimo, Dkt. Kusiluka alibainisha kuwa jitihada za TCDC ni mfano wa kuigwa katika utumiaji wa TEHAMA katika sekta ya ushirika. Alieleza kuwa taasisi zinazotumia mifumo ya kidijitali kama TCDC zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi wa utendaji wa Serikali Mtandao na kuhakikisha udhamini wa shughuli za e-Gov unatekelezwa ipasavyo.
Tume ya TCDC ni miongoni mwa taasisi zinazotambuliwa kitaifa na kuhusiana moja kwa moja na utumiaji wa TEHAMA katika shughuli zake, ikiwemo udhamini wa mikutano, maonyesho, na usimamizi wa vyama vya ushirika. Mfumo huu unalenga kutoa taarifa kwa wakati, kurahisisha upatikanaji wa taarifa, na kusaidia katika maamuzi sahihi yanayolenga kuinua sekta ya ushirika.
Shughuli za kikao cha Serikali Mtandao zinazofanyika Jijini Arusha zinawawezesha wadau wa sekta ya mbalimbali kujifunza, kubadilishana uzoefu, na kuimarisha utumiaji wa teknolojia katika usimamizi wa taasisi za umma. Pongezi za Balozi Kusiluka kwa TCDC zinathibitisha mchango wa taasisi hiyo katika maendeleo endelevu ya sekta ya ushirika nchini.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...