Na Mwandishi Wetu, Karatu.

Umaarufu wa makumbusho hii umeanza kugonga vichwa vya watu na sasa ni zamu ya Tume ya Utumishi wa Umma kutembelea makumbusho hiyo .

Mwenyekiti  wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji mstaafu Hamisa Kalombola ameongoza watumishi hao kuona jinsi maktaba hiyo ilivyohifadhi historia ya dunia kuanzia uumbwaji wa binadamu na mtawanyiko wa miamba na viumbe vingine.

Wakiwa katika Makumbusho hayo wajumbe hao walipata taarifa za kina kuhusu urithi wa kijiolojia, jinsi dunia ilivyoumbwa, vivutio vya asili na utamaduni wa makabila yanayounda Ngorongoro Lengai Geopark ambayo ni hadhi iliyotolewa na UNESCO mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa tume hiyo mhe Jaji Hamisa Kalombola amesema Tume ya Utumishi wa Umma imefurahishwa na namna historia ya Ngorongoro na rasilimali zake ilivyohifadhiwa kwa weledi na ubora wa hali ya juu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Akizungumza na ujumbe huo kwa Niaba ya kamishna wa Uhifadhi, Afisa Uhifadhi Mkuu PCOI Lohi Zacharia ameeleza kuwa Ngorongoro ni kielelezo cha uhifadhi, utalii, maendeleo ya jamii, chimboko la binadamu, urithi wa malikale, eneo lenye uhalisia wa kuwepo kwa wanyama wakubwa watano sambamba na mazalia ya Nyumbu wanaohama ambapo sifa hizo zinastahili kila mtanzania kutembelea Ngorongoro 

Ziara hiyo inalenga kuongeza uelewa wa viongozi na watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za utalii kama nguzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...