Mwaka 1976, Mtafiti wa masuala ya Akiolojia Dr. Mary Leakey aligundua nyayo za zamadamu eneo la Laetoli zilizohifadhika katika mwamba wa jivu la volcano iliyolipuka kwenye milima ya Ngorongoro zaidi ya miaka milion 3.6 iliyopita. Wataalamu wanaamini kuwa nyayo hizo ziliachwa na jamii ya watu wa kale waitwao Australopithecus Afarensis.
Nyayo za Zamadamu Laetoli Ngorongoro ni ushahidi usiopingika kuwa zamadamu (Hominin) wa umri wa miaka milioni 3.66 iliyopita walitembea wima kwa miguu miwili eneo la Laetoli Tanzania.
Kutembea wima kwa miguu miwili kunatutofautisha wanadamu na wanyama kama Sokwe na Nyani waliotokana na babu/bibi mmoja miaka takribani millioni 7 iliyopita.
Uwepo wa Nyayo na masalia ya binadamu, ndege na wanyama, urithi wa utamaduni, mambo kale, mimea, maji, matunda na kila kitu kinachomfanya binadamu kuishi ni kiashiria kuwa pengine bustani ya Eden ni Ngorongoro ni mahali ambapo tunda la mti wa katikati lililiwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...