NA MWANDISHI WETU
ZAIDI ya vikundi 100 vya wajasiriamali wanawake kutoka Mkoa wa Dar es salaam vinatarajia kupata mafunzo ya uwezeshaaji kiuchumi ili kuongeza uelewa na ubunifu.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalumu , Amina Good Said, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo Foundation
Amina amesema mafunzo hayo yatafanyika Februari 13 mwaka huu, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
“Tutayafanya katika Ukumbi wa Blessing uliopo katika Kata ya Segerea. Vikundi zaidi ya 100 vitapata mafunzo hayo bila malipo,”ameeleza .
Amina alieleza mafunzo hayo yatafunguliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Halima Mamuya.
“Ni mafunzo muhimu yatakayo walenga wanawake na makundi yote ya kinamama yanayofanya shughuli za kiuchumi. Tunataka kuwajengea uelewa katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na ubunifu wa shughuli zao,”ameeleza Amina
Alibainisha dhamira ni kuwasaidia wanawake hao kujiongezea kipato na masoko ya uhakika ya bidhaa zao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...