Vyama vya ushirika katika mkoa wa Geita vimeaswa kufuatilia na kujadili madeni kwa kina ili kuepusha vyama hivyo kuelemewa na mzigo wa madeni yanayosababisha vyama hivyo kuanguka kwa kushindwa kukopesheka.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa 8 wa chama kikuu Cha ushirika mkoani Geita GCU uliofanyika February 5 kaimu katibu tawala mkoa wa Geita Charles Chacha aliwasihi wanachama hao kuhakikisha vyama havina madeni yanayofunga fursa mbalimbali za kiuchumi.
Aidha alitoa wito kwa wajumbe wa Bodi kusimamia kwa weledi na uaminifu na kuzingatia wataalamj pale wanapotatizwa na jambo.
" Maswala ya madeni ni mambo ambayo vyama vya ushirika na mikutano mikuu kama hii lipate nafasi ya kujadiliwa kwa kina na kwa uswazi ili kuleta swala Hilo la msingi kwamba tulikopa tunatakiwa kulipa" alisema Chacha .
Vyama vya ushirika mkoani Geita vinakabiliwa na changamoto ya migogoro ya ndani ambapo imeelezwa kuwa vyama vya madini ndio vyama vinavyoongoza kuwa na migogoro ya mara kwa mara kutokana na wanachama kuwa na matarajio makubwa ya mradi kuliko upatikanaji faida.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Geita Doreen Mwanry alisema kuwa kutokana na migogoro hiyo GCU imewashauri wanaushirika wa vyama vya madini kuwa na mwekezaji wa wazi ili panapotokea faida wanachama wote wapate taarifa mapema ili kuepusha migogoro hii.
Chama kikuu Cha ushirika GCU kimeweka mikakati ya kufufua kiwanda Cha kuchambua Pamba kilichopo Kasamwa mkoani Geita, ikiwa ni sehemu za Ahadi alizozitoa rais Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akifanya kampeni mkoani Geita.
Meneja wa GCU Salim Mbwambo alisema kuwa kiwanda hiki kitakapofufuliwa itakuwa fursa nzuri kwa wakulima wa Pamba wa mkoa wa Geita,
Nayo benki ya ushirika imetenga zaidi ya shilingi bilioni 850 kwa ajili ya kuhudumia wana ushirika ambao tayari Wana hisia kubwa katika benki hiyo.
Meneja wa benki ya ushirika Tabu Restut ametoa wito kwa AMCOS za mkoa wa Geita kujitokeza kujiunga na benki hiyo ili waweze kupata mikopo kiurahisi hususani wakulima wa Pamba ambao kwasasa ni kipaombele.




.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...