Na. OWM-KAM - Dar es Salaam.
Waajiri kutoka Sekta Binafsi wametakiwa kuwapa nafasi na kuwazingatia vibarua wanaposajili wafanyakazi kwenye mfumo ili kuweza kutambulika kwenye Mfumo na kuleta tija, usawa katika maeneo ya kazi.
Ameyasema hayo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Ajira na Mahusiano Godwin Mpelumbe wakati akitoa Mafunzo ya Mfumo wa Taifa wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira kwa Waajiri hao Leo Februari 24, 2026 katika Ukumbi wa NSSF Jijini Dar es salaam.
Aidha, Mafunzo hayo yalilenga kuwapatia uwezo katika utoaji taarifa za ajira wakiwa maeneo ya kazi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hata ivyo, jumla ya Waajiri 75 kutoka Sekta Binafsi wameshiriki na kupatiwa Mafunzo ya Mfumo huo ambao utawarahisishia katika upataji taarifa na kujua fursa za kazi zinazotolewa kwenye taasisi mbalimbali.
Kwa upande wa Waajiri kupitia mwakilishi Bi. Hope Lema kutoka Shely's Pharmaceutical Limited ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa elimu kuhusu Mfumo huu kwa sekta binafsi na kueleza kuwa mfumo utasaidia kuingiza taarifa za soko la ajira kwa haraka na wakati wawapo maeneo ya kazi.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...