Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha.

Taasisi ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za pembezoni(MAIPAC) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini jinsi ya kuandika habari zinazochochea amani na kulinda usalama wao wakati wa migogoro.

Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Geita,Mara,Manyara,Mbeya na Arusha,yalidhaminiwa na shirika la wanahabari la Press Unlimited.

Akifungua mafunzo hayo,Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma aliwataka wanahabari kuandika habari ambazo zinahamasisha amani wakati wa migogoro na kuhakikisha wanakuwa salama.

Juma alisema, habari za upande mmoja ambazo hazizingatii maadili na maslahi mapana ya Umma zimekuwa zikisababisha migogoro katika jamii.

Hata hivyo,aliwataka wanahabari wakati wote wa kazi zao kuzingatia usalama wao,kufanya upembuzi yakinifu wa habari wananayotaka kuandika kabla ya kuandika na baada ya kuandika.

"Tujuwe habari ina madhara gani,inafaida gani ,tusiwe na upande katika hiyo habari na kubwa tuwe tunachukuwa tahadhali za kiusalama wa tunapotumia vyombo vya kidigitari na usalama binafsi"alisema

Wakili  wa kujitegemea John Sendodo akitoa mafunzo kuhusu sheria mbalimbali za masuala ya habari ,aliwataka wanahabari kuzingatia sheria hizo hata kama.zinamapungufu.

"Kuna sheria kadhaa ambazo lazima mzijuwe ikiwepo sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 ,sheria ya makosa ya mitandaoni ya mwaka 2015,kanuni.za maudhui mitandao na nyingine kadhaa tusome tujuwe"alisema

Wakili.Sendodo ambaye anafanyakazi na shirika la.kimataifa la Protection Afrika  akifafanua sheria hizo,vifungu kwa vifungu pamoja na mikataba kadhaa ya kimataifa lnayohusiana na wanahabari aliwataka wanahabari kufanyakazi kwa kutovunja sheria lakini wakitekeleza wajibu wao "alisema.

Mmiliki wa Chuo cha waandishi wa habari cha Fanikiwa kilichopo Arusha,Mwanahabari Joseph Mayagilla akitoa mada katika mafunzo hayo, aliwataka wanahabari wakati wote wa kazi zao kuzingatia maadili ya uandishi.

Mayagilla alisema habari za upande mmoja.zimekuwa na madhara katika jamii na sasa kumeibuka uandishi usiojali maadili ya uandishi.

Hata hivyo, alisema ili kuhakikisha habari.zinakuwa bora ni muhimu kurejesha madawati ya vitengo kadhaa kwenye vyombo vya habari ikiwepo madawati ya habari za uchunguzi,amani na maendeleo,uchumi na mengine kwani yataongozwa na waandishi wabobezi wa eneo husika.

Mtaalam wa masuala ya Saikolojia,Ester Cornelio aliwataka wanahabari wanaokabiliwa na msongo wa mawazo kutojifungia kwenye vyombo vya habari na watoke kupata tiba.

Alisema kunywa pombe kupita kiasi ama kuvuta sana sigara hakuwepo kuondoa Msongo wa mawazo (trouma) bali ni kufika kwa wataalam na kupata tiba ambayo ni ushauri.

Cornelio alisema wanaume wamekuwa wahanga wa msongo wa mawazo ama sonona kwa sababu hawazungumzi ili kutoa yaliyomoyoni tofaufi na wanawake.

Wakichangia mada katika mafunzo hayo, Wanahabari Tausi Mbowe ambaye ni meneja wa dawati ya Kidigitali Star Tv,  na Anthony Mayunga kutoka serengeti media, walieleza umuhimu wa maadili ya uandishi na athari za msongo wa mawazo na mapungufu ya sheria.

Tausi Mbowe alishauri kuendelea kuimarishwa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari hasa kuhusiana na sheria na kukabiliana na msongo wa mawazo.

Upande wake mwanahabari Elizabeth Nyivambe kutoka Mbeya na Muta Robet wa Geita na Zakaria Mtigandi wa Manyara walieleza pia umuhimu wa kuendelezwa mafunzo hasa masuala ya matumizi sahihi ya mitandao na usalama kwa wanahabari.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...