Serikali imesema inatilia mkazo katika ulinzi na usalama wa kidijital ili kulinda miundombinu dhidi ya vitisho vya kimtandao ambavyo vinaweza kutumiwa na wahalifu wa ndani na nje ya nchi na kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Akizungumza jijini Dodoma leo Februari 26, 2026 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Angella Jasmine Mbelwa Kairuki wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya wizara na sekta binafsi zilizoko chini ya wizara hiyo wakiwemo TCRA na TTCL,
Waziri Kairuki amesema serikali imeamua kuweka mazingira ya kisera, kisheria na miongozo mbalimbali katika ulinzi na usalama wa Huduma za mtandao kwa kuweka sera nzuri ya uwekezaji, akitolea mfano TCRA na TTCL, na kuwa Wajenzi wa minara ya mashirika hiyo ni wakandalasi wa hapa nchini na kuongeza kuwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania na taarifa zao zinasaidia kuvutia uwekezaji utakao kuwa wa tija kwa Taifa.
Mheshimiwa Kairuki ameyaasa mashirika yaliyoko chini ya wizara hiyo kukamilisha na kutekeleza mipango kabambe kwa mifumo ya Tehama kwa awamu na hasa sehemu zenye pengo kubwa, kuendeleza kukuza uwekezaji wa sekta binafsi kwa kutoa motisha kuweka sheria nzuri na kuwepo na uwazi wa upatikanaji wa ardhi na leseni,kuimarisha usalama wa kidigiti kupitia sera mafunzo na uwekezaji katika vituo vya ulinzi wa kimtandao na upatikanaji wa watoa huduma kwa makundi dhaifu ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika uchumi wa kidijitali.
Kwa upande wake Mchumi mkuu wa Tume ya Taifa Mipango Bwana Jordan Matonya masema kuwa Dira inatoa mwongozo mzuri Kitaifa kwa kupanga na kutekeleza na kuleta muundo na maudhui ya Dira ya 2050 na kuwa na uchumi imara, na kuwa na mpango wa miaka mitano mitano huanzia mwaka huu Julai 2026.
Utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa wa maeneo muhimu ya kiuwekezaji.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...