-Asema waliotambulishwa ni walioingia kwa mara ya kwanza
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ametoa ufafanuzi wa kwanini Rais Dk.Samia Suluhu Hassan hakutambulishwa au kuzungumza wakati wa Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU),uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia
Ufafanuzi wa Waziri Balozi Kombo ameutoa baada ya moja ya mtandao kuandika taarifa ya breaking News kwamba katika hali isiyo ya kawaida na ni aibu Adiss Ababa kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakutambuliwa wala kuruhusiwa kuzungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 39 wa AU.
Akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kwa kina na hatua kwa hatua kuhusu sababu ambazo zimefanya Rais kutotambulishwa.
“Naomba ndugu zangu (waandishi wa habari) muelimishe jamii kuhusu jambo hili, wakuu wa nchi walioruhusiwa kuzungumza ni wale walioingia mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu katika nchi zao.
“Mh. Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amehudumu miaka minne kabla ya Uchaguzi Mkuu kwahiyo kule AU ameshahudhuria mara kadhaa na alishahutubia mara ya kwanza baada ya kifo cha aliyekuwa Rais Dk.John Magufuli.Rais Dk.Samia alihutubia kule…
“Hivyo waliohutubia katika Mkutano wa 39 wa AU ni wale waliongia mara ya kwanza ni zilikuwa nchi tatu ambapo marais wake waliruhusiwa kujitambulisha na kusalimia .Nao ni Gabon ,Ushelisheli na Gine ambao ndio wameingia mara ya kwanza.”
Ameongeza kuwa “ hao walioandika mitandaoni wametafsiri Dk.Samia ameingia AU mara ya kwanza lakini kule ameshazungumza na wanatafsiri miaka minne alikuwepo.
“Kwetu sisi tafsiri yetu sio miaka minne yake kwasababu alıshikilia ule mwaka mmoja Rais kushinda akamalizia ile miaka minne ,kwetu sisi ni mara ya kwanza lakini kule ameshahutubia,”
Katika msisitizo wa ufafanuzi wake Balozi Kombo amesema wakuu wa nchi wale wote waliorudia hawakuzungumza na hivyo sio kwa Rais Samia peke yake bali wako wengi.”Hivyo nimetoa ufafanuzi ili umma ujue sababu yake.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...