KAMPUNI ya ALAF, imezindua Kundi la tano la Mpango wa Wanawake katika Uongozi kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka duniani kote.
Uzinduzi huo, uliofanyika jijini Dar es Salaam uliongozwa na kaulimbiu ya ‘Toa Upate’ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala Msaidi wa Mkoa wa Dar es Salaam-Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Zubeda Masoud ambapo ulikwenda sambamba na wafanyakazi kutambua mafanikio ya wanawake, huku wakionyesha dhamira yao ya uongozi, uwezeshaji na kuisaidia jamii.
Akizungumza katika uzinduzi huo Zubeda aliupongeza uongozi wa ALAF kwa kuwapa wanawake umuhimu unaostahili na kuhakikisha wanashika nafasi za juu za uongozi katika kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kushiriki nao katika Siku ya Wanawake.
“Makampuni mengine yanatakiwa kuiga mfano huu wa ALAF kwani huu ni muendelezo mzuri wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani,” alisema huku akiipongeza kampuni hiyo pia kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalumu ambao walikabidhiwa viti 10 vyenye magurudumu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ALAF, Bibhu Nanda, aliyewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Sateesh Yamsani, alisema kampuni itaendelea kuunga mkono mipango ya wanawake katika uongozi ili kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanapata nafasi za uongozi katika kampuni hiyo.
"Huu unakuwa mpango endelevu ili ALAF iendelee kishika nafasi ya juu katika sekta ya Viwanda kama mwajiri Bora.. tumeona matunda ya mpango huu ulioanza miaka minne iliyopita na kama kampuni tutahakikisha kwamba unakuwa endelevu ili wanawake wengi zaidi waweze kushika nafasi hizi muhimu,”alisisitiza.
Naye Meneja Rasilimali Watu Msaidizi, Rehema Amry alisema: “Huu ni mpango unaolenga kuimarisha uwezo wa uongozi na kusaidia ukuaji wa kitaaluma wa wanawake ndani ya kampuni.”
Alisema maadhimisho ya mwaka huu yana umuhimu wa kipekee kwani ALAF inaadhimisha miaka 65 ya ubora, ubunifu na mchango katika maendeleo ya viwanda Tanzania. “Katika miongo sita iliyopita, kampuni imeendelea kukuza ukuaji jumuishi na kutoa fursa kwa watu wake na jamii inayowahudumia,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Rehema, ALAF inapoendelea na safari yake ya ukuaji na matokeo yake chanya kwa jamii, inathibitisha dhamira yake ya kujenga mahali pa kazi shirikishi, ambapo wanawake wanawezeshwa kuongoza, kuhamasisha na kuchangia katika maisha bora ya baadaye.
“ALAF, tunaamini kwamba kuwawezesha wanawake na kuzisaidia jamii zetu kunakwenda sambamba hivyo tunaposherehekea miaka 65 ya ubora, tunaendelea kujitolea kutengeneza fursa kwa wanawake kuongoza, huku tukifanya mabadiliko ya muhimu katika jamii kwani hisani huanzia nyumbani.”
Wakati huo huo, katika ari ya kutoa kwa jamii, wafanyakazi wanawake ALAF walichangia kwa hiari kusaidia ajenda ya kampuni ya uwajibikaji kwa jamii. Kwa juhudi zao za pamoja, viti 10 vya magurudumu vilitolewa kwa watoto wenye mahitaji maalumu, huku kiti kimoja cha magurudumu kikikabidhiwa kwa mfanyakazi wa ALAF, na kusisitiza imani kwamba hisani huanzia nyumbani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...