Mkurugenzi Mtendaji wa Benkiy a Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa sita kushoto), akionesha tuzo ya ‘Rising Women’ mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (wa tano kushoto), jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo ilitambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wanawake, kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na kuunda fursa zenye maana kwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akikabidhi tuzo ya ‘Rising Women’ kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bww. Obedi Laiser (wa pili kulia), jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo ilitambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wanawake, kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na kuunda fursa zenye maana kwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akikabidhi tuzo ya shukrani kwa Meneja Huduma za Jamii na Mtukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika Mpango wa Rising Women. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo ilitambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wanawake, kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na kuunda fursa zenye maana kwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa nne kushoto), na Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa wa benki hiyo, Bi. Abigail Lukuvi (wa tatu kulia), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Absa, wakipozi na tuzo za utambuzi za ‘Rising Women’ jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo ilitambuliwa kwa dhamira yake thabiti ya kuwawezesha wanawake, kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na kuunda fursa zenye maana kwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...