CHIFU wa Kibondo mkoani Kigoma Mama Mwamvua Rajab Ruhaga Nyamaliza amefariki dunia ghafla asubuhi ya tarehe 24 Machi 2026 akiwa msibani Malinyi, mkoani Morogoro.

Taarifa za kifamilia zinaeleza kuwa marehemu alikuwa amesafiri kwenda Malinyi kuhudhuria mazishi ya binti yake, Zubeda Juma Ruhaga, kabla ya kifo chake hicho cha kushtukiza kutokea.

Kifo hicho kimeacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wakazi wa Kibondo, ambako marehemu alikuwa akihudumu kama kiongozi wa kimila na mshauri muhimu wa jamii.

Kwa sasa, familia ipo katika maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Morogoro kuelekea Kibondo, Kigoma, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia kadri mipango inavyoendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...