Farida Mangube Morogoro

Kampuni ya Coca-Cola imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 5 katika mradi wa kulinda na kurejesha vyanzo vya maji vya Bonde la Wami-Ruvu, hatua inayolenga kunufaisha zaidi ya wakulima 2,000 wanaotegemea rasilimali hiyo kwa maisha na shughuli zao za kiuchumi.

Fedha hizo zimewekezwa kwenye Mradi unaojulikana kama NBS4WATER unatekelezwa na IUCN kwa kushirikiana na Serikali kupitia Bodi ya Maji ya Bonde la Wami-Ruvu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Coca-Cola katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, kuhifadhi mazingira, na kusaidia wakulima kutumia mbinu Bora za kilimo zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi mjini Morogoro, Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, David Chait, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya dhamira ya kampuni hiyo kuhakikisha maji yanapatikana kwa shughuli za kiuchumi.

“Bonde la Wami-Ruvu lina mchango mkubwa kwa maisha ya watu na uchumi wa taifa. Kulinda vyanzo vyake ni jukumu letu sote,” alisema Chait.

Kwa Meneja wa mradi kutoka IUCN, Doyi Mazenzele, amesema zaidi ya wakulima 2,000 watanufaika moja kwa moja kwa kufundishwa kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku mradi ukitarajiwa kurejesha zaidi ya hekari 3,000 za ardhi na kuongeza upatikanaji wa maji kwa lita milioni 548.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara hiyo, Rosemary Rwegubisa, amesema serikali imepiga marufuku shughuli zote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji, huku hatua mbadala ikiwemo upandaji miti, ufugaji wa nyuki na uchimbaji wa visima, ili wananchi waweze kujipatia kipato bila kuharibu mazingira.

Kaimu Mkurugenzi wa Bonde la Wami-Ruvu, Juvenalis Tarimo, alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kulinda rasilimali hizo, akibainisha kuwa mafanikio ya mradi yataegemea ushirikiano wa karibu na jamii.

Makamu wa Rais wa Coca-Cola Afrika Mashariki na Kati, Alfred Olajide, alisema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kimataifa za kampuni hiyo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji duniani.

Uzinduzi huo uliambatana na zoezi la upandaji miti zaidi ya 2,000 kando ya Bwawa la Mindu mjini Morogoro, ikionyesha kuanza kwa utekelezaji wa hatua za vitendo katika kulinda na kurejesha vyanzo vya maji.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...