Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amefungua mkutano wa kitaifa unaowakutanisha wadau wa taasisi za utafiti kwa lengo la kujadili namna bora ya kuoanisha tafiti na mchakato wa upangaji wa maendeleo ya taifa.
Mkutano huo wa siku mbili umeanza Machi 23, 2026 jijini Dodoma, ukihusisha watafiti, watunga sera na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Dkt. Kida amesema Tanzania ipo katika hatua muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi wa thamani ya trilioni moja pamoja na kuboresha ustawi wa wananchi.
Amefafanua kuwa dira hiyo inalenga pia kutokomeza umasikini uliokithiri, kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi, na kupunguza vifo vya watoto wachanga ifikapo mwaka 2050.
“Tutahakikisha hakuna Mtanzania atakayebaki katika umasikini uliokithiri, huku tukiboresha huduma muhimu za kijamii kama afya na elimu,” amesema Dkt. Kida.
Aidha, ameeleza kuwa utekelezaji wa dira hiyo utaongozwa na mipango ya muda mrefu itakayogawanywa katika vipindi vya miaka mitano mitano, huku kila mwaka ukiwa na mpango mahsusi wa utekelezaji wenye vipaumbele vya kitaifa.
Amesema Tume ya Taifa ya Mipango itaendelea kuwa mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya uchumi na maendeleo, sambamba na kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mipango hiyo.
Akigusia umuhimu wa tafiti, Dkt. Kida amesisitiza kuwa tafiti za kiuchumi na kijamii ni nyenzo muhimu katika kubuni sera bora, kuimarisha utekelezaji wa mipango, na kufikia malengo ya maendeleo ya taifa.
“Ni muhimu kuwa na mwongozo madhubuti wa tafiti unaozingatia vipaumbele vya taifa ili kuhakikisha matokeo yake yanatatua changamoto halisi za wananchi,” amesisitiza.
Katika kuimarisha ushirikiano na wadau wa utafiti, Dkt. Kida amesema Tume ya Taifa ya Mipango inapanga kuanzisha mfumo wa kidijitali (portal) wa kuhifadhi na kusambaza tafiti zote zinazofanyika nchini, ili kuhakikisha zinatumika kikamilifu katika maamuzi ya kisera na mipango ya maendeleo.
Ameongeza kuwa tafiti hizo zitakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi, jamii na mazingira, hasa katika kukabiliana na changamoto zinazoibuka kama ongezeko la idadi ya watu na mabadiliko ya tabianchi.
Mkutano huo unalenga kujenga uelewa wa pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za utafiti, ili kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zinaendana na vipaumbele vya maendeleo ya taifa.
Kwa ujumla, Tanzania inaendelea kujipanga kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii, yakilenga kujenga uchumi shindani na jumuishi, kuongeza ajira na tija, pamoja na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya taifa.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...