Serikali imeitaka Taasisi ya Elimu Tanzania kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa tathimini ya utekelezaji wa  mitaala iliyoboreshwa ili kuleta matokeo chanya katika jamii.

Hayo yamesemwa leo tarehe 4/3/2026 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Mhe. Wanu Hafidh Ameir alipofanya ziara ya siku moja katika taasisi hiyo ili kupata uelewa wa majukumu mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo katika kuchangia ukuaji wa Sekta ya Elimu nchini. 

“Nashukuru kwa taarifa yenu ya utakelezaji wa majukumu malimbali ambayo inatoa picha halisi ya kazi kubwa inayofanywa TET, hivyo pia nawaomba muimarishe kufanya tathimini  ya utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa ili kama kuna changamoto ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka.” Amesema Mh.Wanu.

Sambamba na hilo Mhe. Wanu amepongeza juhudi za utekeleaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023) na mitaala iliyoboreshwa mwaka 2023 kwa vitendo, na kusema kuwa, inaonesha dhamira ya dhati katika kuimarisha ubora na mwelekeo wa elimu nchini.

Pia, Mhe. Wanu ameipongeza TET kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uzalendo, hususan katika kuboresha maudhui ya ujifunzaji kwa watoto wadogo kupitia katuni zenye maadili  na tamaduni za Kitanzania.

Akieleza majukumu yanayotekelezwa na TET,  Mkurugenzi Mkuu Dkt. Aneth Komba amesema TET  kwa kushirikiana na wadau wa elimu, inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za elimu zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali katika eneo la ufundishaji na ujifunzaji.

Pia  Dkt. Komba ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za kutosha na kwa wakati zinazosaidia katika eneo la uandishi wa  vitabu, uchapaji na usambazaji katika shule zote nchini. 













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...