NA MWANDISHI WETU, CHWAKA

Katika kuboresha sekta ya elimu  Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mhe. Issa Gavu leo Machi 25,2026 amekabidhi vitabu kwa ajili ya kujisomea pamoja na vifaa mbali mbali vya elimu, lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko katika kukuza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa skuli  zote la Jimbo hilo.

Akikabidhi msaada huo Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Mhe Gavu amebainisha kwamba wameamua kutoa msaada wa vifaaa mbali mbali kwa wanafunzi hao ikiwemo kompyuta mpakato,Printer, vitabu mbali mbali pamoja na mashine ya kuburuzia karatasi (Photocopy mashine)  vyote vikiwa vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 12,msaada ambao umetolewa kutoka kwa marafiki wema kwa watu wa Jimbo la Chwaka.

"Leo tumejumuika hapa kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbali mbali kwa wanafunzi ambao wanasoma katika Jimbo la Chwaka na katika siku ya leo tumekabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo vitabu kwa ajili ya kujisomea wanafunzi, Photocopy mashine, pamoja Printer ambavyo vitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi kuweza kuongeza kasi ya ufaulu katika masomo yao,"amebainisha Mhe. Gavu.

 Aidha katika tukio hilo pia Mhe. Gavu kwa kushirkiana na marafiki zake wa Jimbo hilo pia wametoa msaada wa  kugawa  mabati katika  Skuli ya Mrembo Uroa,Mashine ya kufulia nguo (Washing Machine), tanki  la maji na mipira Jendele, pamoja na mafeni na vifaa vya umeme kwa Kituo cha Afya Cheju.

Gavu amesema  kwamba wameamua kutoa misaada hiyo katika nyanja mbali mbali ikiwa ni moja ya hatua ya kuimarisha suala la  elimu kwa wanafunzi  pamoja na kuboresha afya kwa jamii ambayo inawazunguka hasa katika Jimbo la Chwaka na kuwasihi wanafunzi wasome kwa bidii,lengo ikiwa ni kuongeza maarifa  ambayo yatawasaidia katika siku za usoni.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...