
LIGI kuu ya Tanzania inazidi kupamba moto huku mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania Yanga wameendelea kujikita kileleni huku wakionesha nia yao ya kubeba taji hilo.
Mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Yanga wanaendelea kuonesha uimara wao kwenye Ligi Kuu za Tanzania yaani (NBC), wakishikilia nafasi ya juu kwenye msimamo wakiwa na pointi zao 29 hadi sasa.
Tangu kuanza kwa msimu, Yanga wamekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo, wakionyesha ubora mkubwa katika safu ya ushambuliaji pamoja na nidhamu ya kiuchezaji iliyowafanya kuwa timu ngumu kufungika huku mpaka sasa wakiwa hawajapoteza mchezo wowote kwenye ligi.
Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mkuu Pedro Goncalves wanatarajiwa kuwa na mafanikio msimu huu ya kuchukua makombe makubwa ikiwemo la ligi kuu ya Tanzania kwani ana wachezaji wazuri sana.
Wachezaji wao muhimu wameendelea kubeba majukumu ipasavyo, huku wakifanya ongezeko la wachezaji msimu huu wakiwemo Allan Okelo, Depu, Damaro, Mwanengo, Buba na wengine wengi.
NB: Mbali na kubashiri mechi za kandanda, Meridianbet pia inakupa nafasi ya kucheza michezo ya kasino mtandaoni kama Aviator, Keno, Super Heli, ambapo unaweza kujishindia zawadi kama simu mpya aina ya Samsung A26. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
Hata hivyo, safari yao kimataifa haikuwa na matokeo yaliyotarajiwa. Katika michuano ya CAF Champions League, Yanga walipambana kwa nguvu lakini walishindwa kuvuka hatua inayofuata ya Robo Fainali.
Ushindani mkali wa kimataifa, uzoefu wa wapinzani pamoja na changamoto za nje ya uwanja uliwafanya washindwe kuendelea mbele kwenye michuano hii huku wakiishia hatua ya makundi kama wenzao Simba. Jisajili hapa kwani ODDS KUBWA zinakungoja wewe.
Japokuwa kutolewa huko hakufuti mafanikio yao ya ndani, bali kumetoa funzo na uzoefu muhimu kwa kikosi. Yanga wameonyesha kwamba wana uwezo wa kushindana katika viwango vya juu, lakini bado kuna maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kufikia malengo makubwa barani Afrika.
Kwa sasa, nguvu zote zimeelekezwa katika kuhakikisha wanadumisha ubora wao kwenye ligi na kutetea taji lao. Malengo ni wazi kumaliza msimu wakiwa kileleni na kurejea tena kwenye michuano ya kimataifa wakiwa imara zaidi, wakiwa na uzoefu wa kutosha wa kukabiliana na presha ya mashindano ya juu.
Je vijana hawa wa Jangwani wanaweza kutetea taji lao msimu huu?. Au wanaweza wakabeba mataji mangapi msimu huu wa 2025/26. Bashiri hapa na Meridianbet.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...