JIMBO la Vunjo limezindua kampeni maalum ya upandaji miti katika jimbo hilo ikiwa ni mkakati wa kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. 

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo, uliofanyika katika shule za sekondari za Mwika Kata ya Mwika Kaskazini, shule ya sekondari Mieresini kata ya makuyuni na shule ya sekondari ya amali ya Koresa kata ya Kirua vunjo kusini, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha miti inayopandwa inatunzwa kwa uangalifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Alielekeza kuwa kila mwanafunzi anayekabidhiwa mti anapaswa kuwa na wajibu wa kuutunza hadi atakapomaliza masomo yake, hatua inayolenga kujenga uwajibikaji wa moja kwa moja katika utunzaji wa mazingira.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola aliahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira. 

Alisisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusambaza miche ya miti na kupanua wigo wa kampeni hiyo katika maeneo mengine ya jimbo hilo ambapo alitumia pia nafasi hiyo kutoa  shukrani kwa wadau wote walioshiriki na kuunga mkono zoezi hilo.

Aidha, alipanda miti kama ishara ya uongozi kwa vitendo na kuahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira. 

Katika uzinduzi huu, Mbunge wa viti maalum kupitia Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dkt.Catherin Joachim, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya, Hussein Jamal pamoja na madiwani wa Kata za Makuyuni Dickson Tarimo, Samwel Shao wa Mwika Kaskazini na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Geoffrey Mkunde wa Kirua Vunjo Kusini pamoja na Diwani viti Maalumu Pamela Lazaro walishiriki katika uzinduzi huu.  








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...