Na. Philipo Hassan - SERENGETI
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA Mussa Nassoro Kuji, leo Machi 01, 2026, amefanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa lengo la kukagua hali ya miundombinu kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya hifadhi hiyo.
Katika ziara hiyo, Kamishna Kuji alitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hususan barabara ya kutoka Seronera kuelekea Nabii, ambapo eneo la kivuko cha Viboko cha Nabii limeathirika kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha maji. Hali hiyo imepelekea magari ya waongoza watalii pamoja na watumiaji wengine wa barabara kulazimika kusubiri kwa muda ili kuruhusu maji kupungua katika baadhi ya vivuko kabla ya kuendelea na safari.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Kamishna Kuji alisema kuwa TANAPA itaendelea kuhakikisha kuwa miundombinu ya hifadhi inaboreshwa ili kubaki kuwa salama na kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa barabara.
“Mvua zinazoendelea kunyesha zimeleta changamoto katika baadhi ya maeneo ya barabara, nimeielekeza Menejimenti ya hifadhi kuchukua hatua za haraka kuboresha vivuko vilivyoathiriwa pamoja na kufanya tathmini ya kina ya barabara yote ya Seronera hadi Nabii ili kuhakikisha usalama wa watalii na watumiaji wengine wa hifadhi,” alisema Kamishna Kuji.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Izumbe Msindai alipokea maelekezo kutoka kwa Kamishna Kuji na kueleza kuwa uongozi wa Kanda kwa kushirikiana na hifadhi utaendelea kuimarisha miundombinu ya hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha huduma za utalii zinaendelea kutolewa kwa usalama na ufanisi hata katika kipindi cha mvua.
“vikosi maalumu vya kukwamua magari na kutoa maelekezo vipo maeneo mbalimbali ili kuhakikisha tunalinda usalama wa wageni na mali zao sambamba na kutoa huduma muda” alieleza Kamishna Msindai.
Aidha, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Ismail Omary Ismail ambaye pia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, amewataka watumiaji wa barabara hususan waongoza watalii kuzingatia tahadhari wanapokuwa ndani ya hifadhi.
“Tunawasihi waongoza watalii na watumiaji wote wa barabara kuendesha magari kwa tahadhari kubwa na kufuata maelekezo yanayotolewa na Maafisa na Askari wa Uhifadhi, hasa katika kipindi hiki cha mvua, ili kuepusha ajali na madhara yanayoweza kujitokeza,” amesema Kamishna Ismail.
Ziara hiyo iliambatana na ukaguzi wa huduma za utalii ambapo Kamishna Kuji alifanya ukaguzi katika lango la kuingilia watalii la Nabii na kujionea watalii wengi wakiingia na kutoka katika hifadhi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...