Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi amemsifia na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Itilima mkoani Simiyu Njalu Silanga kwa namna anavyowasilisha bungeni hoja zenye mashiko na zenye kulenga kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Kihongosi amesema mbunge huyo ameonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wake kwa kusimamia masuala muhimu ya maendeleo na kuyapeleka kwa nguvu bungeni ili kupata ufumbuzi.

Ametoa pongezi hizo Machi 8 wakati Kenani Kihongosi alipotembeleq na kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Itilima mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi katika Kanda ya Ziwa.

Kutokana na juhudi hizo, Kihongosi amewataka wananchi wa Jimbo la Itilima kuendelea kumuamini na kumuunga mkono mbunge wao ili aweze kuendelea kupigania maendeleo yao kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wao, wananchi wa Jimbo hilo wameonesha furahiq na kuridhishwa na kazi inayofanywa na mbunge wao, wakimpongeza kwa kuwaletea maendeleo mbalimbali jimboni humo ikiwemo ujenzi wa shule, vituo vya afya pamoja na kusambazwa kwa huduma ya umeme katika maeneo tofauti ya jimbo hilo.

Pia wamemshukuru mbunge huyo kwa kujali ustawi wa jimbo lao na kumuombea aendelee kuwa na nguvu na moyo wa kuwatumikia ili maendeleo yaendelee kuongezeka katika Jimbo la Itilima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...