🎈 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akaribisha kuwekeza Iringa
🎈NSSF yatoa elimu kwa wadau, wataka wajiunge wafaidike na Mafao
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James
amefungua Kongamano la MISA TAN WADAU SUMMIT 2026 ambao umewakutanisha waandishi wa habari, wahariri na wadau wa habari ambapo amesema serikali ya Mkoa wa Iringa itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa haki kupata habari.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amesema kongamano hilo litumike pia kuelezea fursa za kiuchumi ambazo zinapatikana kwa Mkoa wa Iringa ikiwemo uwekezaji wa viwanda ,sekta ya kilimo na sekta ya utalii .
Katika hotuba yake, James ametumia fursa hiyo kuitangaza Iringa kama kitovu kipya cha uwekezaji nchini, akieleza kuwa uchumi wa mkoa huo umeongezeka kwa kasi kutoka Sh trilioni 4.5 mwaka 2020 hadi kufikia zaidi ya Sh trilioni 6.3 mwaka 2024.
Amesema ukuaji huo umetokana na jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, misitu, mifugo, viwanda pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya barabara, maji na umeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania MISA TAN Edwin Soko amesema MISA TAN imejipanga kujenga Kituo cha kusambaza habari za maendeleo ambacho kitatoa nafasi ya wadau mbalimbali kujua taarifa za kimaendeleo zinazofanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku Mkuu wa Mkoa wa Iringa amekubali kutoa kiwanja kwaajili ya kujengwa kwa kituo hicho.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema pamoja na hilo, taasisi hiyo inaendelea kuhamasisha uandishi wa habari wenye mwelekeo wa suluhisho ili kusaidia jamii kupata majibu ya changamoto zinazowakabili.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema Benjamin Sitta amewata wananchama wa MISA TAN ambao ni waandishi na wahariri kuendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari katika kubadilisha fikra za vijana katika kubuni
Fulsa za kiuchumi.
Katika kongamano hilo wadau mbalimbali walishiri ikiwemo mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF kupitia Elizabeth Mwakanye , ampapo ametumia jukwaa hilo kuelezea kazi zinazofanywa na NSSF na kuwata wenye sifa za kujiunga na mfuko huo waweze kujiunga ili kitoa nafasi ya kufaidika na mafao yakiwemo mafao ya matibabu, uzazi, na pensheni ya uzee na mafao mengine yanayotolewa na mfuko huo.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...