Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewashauri viongozi kujenga utamaduni wa kuwasaidia wananchi hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuweka uwiano sawa wa mahitaji.

Ametoa wito huo mara baada ya zoezi la kuwagawa Iftar kwa  wananchi wa jimbo la kiwani shehia ya kendwa yenye nyumba zaidi ya 1156 hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mauuwani Jimbo la Kiwani.

Amesema ataendeleza utamaduni wake wa  kugawa Iftari kwa wananchi wote hasa wenye mahitaji Maalum ili kupunguza ukali wa maisha na kupata chakula katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amefahamisha kuwa  mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni Maalum kwa waumini wa Dini ya kiislamu kufanya matendo mema  yanayompendeza Mwenyezi Mungu,hivyo ni vyema kwa kila mwenye uwezo kutoa na kuwapa wahitaji ili kupata fadhila zilizomo ndani ya mwezi huu.

Aidha, Mhe. Hemed amesema anatarajia kuzifikia shehia zote saba ( 7 )  zilizomo ndani ya Jimbo hilo na kuzipatia Iftari jambo ambalo litaongezea umoja na mshikamano kwa wannachi wa jimbo hilo.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaomba wafanya biashara kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiweo Masikini, Wajane, Mayatima na watu wasiojiweza hasa katika mwezi mtukufu wa ramadhani ili kuzidi kuzitakada biashara zao na kupata fadhila zilizomo ndani ya mwezi wa ramadhani.

Kwa upande wake mfanya biashara SAID NASSIR NASOR ( BOBAR ) ameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kumpatia ushirikiano ambapo kwa mwezi huu wa ramadhani amepatiwa  usafiri wa kusafirisha bidhaa mbali mbali  ambazo atawakabidhi wananchi wa kisiwani Pemba wakiwemo waannchi wa jimbo la kiwani.

Amesema kuwa lengo lake ni kuwafikia  wananchi mbali mbali wasio na uwezo kwa Unguja na Pemba ili kila mwananchi apate sadaka  itakayowasaidia kwa Iftari lakini pia aweze kupata fadhila hapa duniani na kesho akhera.

Nao wananchi waliopatiwa sadaka hizo wamemshukuru mwakilishi wao kwa kuendelea kuwatumikia kwa  moyo wa upendo,  huruma na usawa kwa wananchi wote jimboni humo jambo ambalo linawapa faraja na imani kubwa juu yake.

Wamesema hawana shaka na utendaji kazi wa Mhe. Hemed na matumaini yao makubwa ni kuzidi kuwaletea maendeleo jimbo humo kama vile alivyoanza kuzitekeleza ahadi mbali mbali alizoziahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwa mwakilishi wa Jimbo la Kiwani.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...