Na Seif Mangwangi,  Michuzi TV Arusha

WAKUU wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika ambazo bado hazijaridhia itifaki ya uanzishwaij wa mahakama ya Afrika ya  Haki za binaadam na Watu(AfCPHR),  wametakiwa kuharakisha itifaki hiyo Ili kuruhusu Haki na demokrasia kutendeka katika nchi zao.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mwaka wa mahakama ya Watu na Haki za binaadam 2026 pamoja na maadhimisho ya miaka20 tangu kuanzishwa Kwa mahakama hiyo leo 2Machi 2026,  Rais wa Jamhuri ya Ghana, John Dramani Mahama amesema hakuna jambo la kuogopa Kwa kuwa mahakama hiyo Ina lengo la kutenda haki pekee.

Amesema Baba yake ambaye alishawahi kuwa Waziri katika utawala wa Rais Kwame Nkuruma alishawahi kuwekwa kizuizini Kwa zaidi ya miaka 14 kwa kusema ukweli na baadae kuachiliwa lakini kungekuwa na mahakama hiyo familia ingeweza kufikisha mashtaka katika mahakama hiyo.

“ Nipende kutoa wito kwa wakuu wa nchi ambazo bado hawajaridhia itifaki ya mahakama hii kuridhia Kwa kuwa hakuna cha kuogopa, waridhie Ili kuwezesha wananchi wao pamoja na asasi za kiraia kufikisha malalamiko Yao pale wanapoona Sheria hazijafuatwa,” amesema.

Amesema ukiukwaji wa Haki za binaadam husababisha athari kubwa kwa familia na jamii na hivyo uwepo wa mahakama hiyo husaidia kupatikana kwa haki dhidi ya wale ambao wamekuwa wakizikiuka.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binaadam na Watu,  Jaji Blaisse Tchikaya amesema katika kuadhimisha miaka 20 ya mahakama hiyo, bado kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo watu wengi kutofahamu majukumu ya mahakama hiyo.

Aidha amesema  upungufu wa fedha umekuwa ni kikwazo kingine kinachosababisha mahakama hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa elimu Kwa wadau wa mahakama hiyo.

“Wakati tunaadhimisha miaka 20 ya mahakama bado tunakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitajii ufumbuzi wa haraka Kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali hususani wakuu wa nchi, mfano Afrika tuna nchi 55 lakini zilizoridhia itifaki ya mahakama hii ni nchi 35 pekee, utaona hapa bado Kuna kazi ya kufanya,” amesema  Jaji  Tchikaya.

Amesema changamoto nyingine ni  nchi wanachama kushindwa kutekelezaji maamuzi yanayoamuliwa na mahakama hiyo jambo ambalo limekuwa likififisha demokrasia na kurudisha nyuma malengo ya kuanzishwa Kwa mahakama hiyo.





Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Ally Posi amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kufanyiakazi itifaki ya kuruhusu asasi za kiraia kuweza kufikisha mashauri yao katika mahakama hiyo baada ya kujiondoa katika kipengele hicho.

Hata hivyo Wakili Dkt Posi amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa msaada wake kwa mahakama hiyo kwa kuwa ni chombo kilichoanzishwa Kwa lengo la Kukuza demokrasia katika bara la Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...