Na Wizara ya Madini
Kabla ya mwaka 2019, biashara ya madini ya dhahabu na vito nchini Tanzania, hususan kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara, ilifanyika bila kuwepo kwa maeneo rasmi ya kukutana. Hali hiyo ilisababisha kutokuwepo kwa uwazi katika bei, udanganyifu katika vipimo na ubora wa madini, uwepo wa dhahabu bandia, pamoja na vitendo vya utoroshaji wa madini nje ya nchi, jambo lililosababisha wachimbaji na wafanyabiashara kupata hasara na Serikali kukosa mapato stahiki.
Mageuzi makubwa yalianza mwaka 2019 baada ya kufanyika marekebisho ya Sheria ya Madini mwaka 2017, ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa soko la kwanza la Madini Geita likifutiwa na Chunya. Hatua hiyo iliweka msingi wa uwazi, usalama na uhakika wa biashara ya madini.

Leo, Tanzania ina masoko 44 ya madini na vituo vidogo vya ununuzi wa madini 120 nchi nzima. Masoko haya yamekuwa mkombozi mkubwa kwa wachimbaji na wafanyabiashara kwa kuwapatia mahali salama pa kuuza, bei elekezi na ulinzi dhidi ya udanganyifu huku Serikali ikipata mapato yake stahiki.
Uwepo wa masoko ya madini na vituo vidogo vya ununuzi wa madini umepelekea wimbi kubwa la watanzania kuingia kwenye uchumi wa madini, hususan uchimbaji mdogo huku mifumo rafiki, uwazi na uhakika wa kisheria wa kuchimba na kufanya biashara vimeifanya Tanzania kuwa chaguo bora kwa wachimbaji wadogo barani Afrika na wageni kufika kujifunza.

Tayari nchi kama Zambia, Malawi, Burundi, Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zimefika kujifunza kuhusu mfumo huo na hivi karibuni nchi ya Bukinafaso ilifika kujifunza.
Takwimu zinaonesha wazi mafanikio ya mfumo huo kabla na baada ya masoko kuanzishwa ambapo mwaka 2018/19 mauzo ya madini kupitia mfumo wa masoko yalifikia shilingi bilioni 8 kwa mwaka, ambapo awali fedha hizo zilipotea. Mwaka wa 2021/22 mapato kupitia masoko pekee yalifikia shilingi bilioni 264.09 na mwaka 2023/24 biashara ya thamani yenye shilingi trilioni 2.095 na trilioni 1.926 mtawalia ilifanyika kupitia masoko hayo. Hali hiyo inaonesha mwenendo chanya na endelevu wa mapato ya Serikali kupitia masoko ya madini.
Mathalani, Mkoa wa kimadini Chunya, uwepo wa masoko ya Madini umeongeza chachu ya uzalishaji wa dhahabu ambapo Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kimadini Chunya Mhandisi Laurent Mayalla akizungumza na Madini Diary anasema kuna ongezeko la shughuli za madini ambazo zimeleta mageuzi makubwa na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta nyingine. Anasema uzalishaji wa madini ya dhahabu hivi sasa umefikia kilo 300 kwa mwezi kutoka kilo 5 zilizokuwa zikizalishwa kabla ya masoko.
Kupitia kodi na tozo mbalimbali, mapato haya yanarejea kwa wananchi kwa kugharamia huduma za jamii na miradi ya maendeleo jambo linaloifanya rasilimali hii kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa taifa kwa ujumla, na hii ndiyo tafsiri nyingine ya kauli kwamba: madini ni maisha na madini ni utajiri, uchumi na maendeleo.
Masoko ya Madini Yachochea Maendeleo ya Halmashauri
Kutokana na umuhimu wa miundombinu hii, Serikali za Mitaa zimeendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya masoko kutokana na manufaa yanayoonekana wazi kwa wananchi. Masoko yamezalisha ajira lukuki kwa vijana kupitia biashara, usajili na huduma mbalimbali.
Mfano mdogo ni pale unapofika sokoni, unakutana na makundi ya vijana wakiwa na dhahabu mikononi, wakipokea kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara kwa ajili ya kusajiliwa ili kuuzwa. Taswira hii inaonesha wazi kuwa masoko ya madini yameunda mnyororo mzima wa thamani, unaogusa wachimbaji, wafanyabiashara, vijana na Serikali kwa ujumla.
Kwa ujumla, masoko ya madini yamebadilisha taswira ya sekta kutoka biashara ya dhahabu na vito kiholela kwenda mfumo wa uwazi, unaosimamiwa kwa karibu na Serikali ambapo kila shilingi ya Tanzania inayoingia inaonekana. Si ajabu kuwa nchi nyingi za afrika zimekuja kujifunza uzoefu wa Tanzania na hii ndiyo tafsiri halisi kwamba madini ni maisha na madini ni utajiri.
Pia, ndiyo tafsiri kwamba Serikali inasikiliza na inapokaa mezani na wadau inachukua hatua kwa vitendo. kupitia Sera, mabadiliko ya mifumo na uanzishaji wa masoko ya madini, Serikali imehakikisha sekta ya madini inafikika kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara, huku ikileta matokeo yanayoonekana wazi katika uwazi wa biashara, ongezeko la ajira na mapato ya taifa na usimamizi madhubuti.
Kwa mafanikio haya, masoko ya madini yanaendelea kudhihirisha kuwa rasilimali za madini si tu chanzo cha mapato, bali pia ni daraja la fursa, ajira na maendeleo kwa watanzania wengi.
#Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...