Na Diana Byera, Bukoba
MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhandisi Johnstone Mtasingwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamefanikisha kununua mashine ya kudurufu mitihani katika Shule ya Msingi Bunena iliyoko Manispaa ya Bukoba baada ya zoezi hilo kukwama miaka mitano iliyopita.
Wadau wengine walioshiriana na Mbunge Mtasingwa ni Diwani wa kata Bakoba Shabani Rashidi, wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Bunena Manispaa ya Bukoba
Wanafunzi, Wazazi, walezi na uongozi wa shule wamepokea mashine hiyo ya kudurufu mitihani (Photocopy mashine) yenye thamani ya Shilingi 3,400,000 na kutoa pongezi kwa wadau wa maendeleo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini ambaye alipokea kilio hicho wakati wa kampeini zake za kugombea ubunge na sasa anaendelea kushirikiana na wadau kutimiza haadi zake
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge huyo wakati wa kukabidhi mashine hiyo Katibu wa Mbunge Hamada Simba amesema pia amepokea maombi ya kompyuta mbili za kuchapisha mitihani katika shule hiyo ambapo amesema atanunua kompyuta hizo haraka.
Amesema kuwa lengo ni kufanya wanafunzi wa shule hiyo kuzoea mitihani iliyochapishwa na kupunguza adha kwa wazazi na walezi wa wanafunzi
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bakoba Shaban Rashid ametoa pongezi kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Kata na ofisi ya Mbunge wa Jimbo kuhusu changamoto mbalimbali ambazo amezitatua kwa miezi mitano tangu amechaguliwa na kwamba Mbunge huyo amekuwa akijituma na anawafikia wananchi Haraka.
“Wananchi waendelee kumpa ushirikiano katika utendaji wa kazi na hadi kufikia miaka mitano watakuwa wamepata manufaa makubwa kupitia utendaji kazi wa Mbunge huyo.”
Awali Mwalimu Muu wa Shule ya msingi Bunena Devotha Mugisha amesema imewachukua wazazi miaka mitano kuchangia mashine hiyo lakini baada ya Kuona mwitikio wao Mbunge na diwani wameunga mkono jitihada zao.
Ambapo ametoa shukuran kwa viongozi hao na kuhaidi watoto watakaomaliza Darasa la Saba mwaka huu wengi wao watachaguliwa katika shule za vipaji maalumu.
Amesema shule hiyo ni miongoni mwa shule Kongwe ambayo ilianza mwaka 1902 na changamoto kubwa kwa sasa ilikuwa vifaa vya tehama jambo ambalo limetatuliwa.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya Sita imekarabati shule hiyo ambayo hapo mwanzo ilijengwa kwa udongo na sasa inamazingira mazuri ya watoto kujifunzia.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...