Na Diana Byera,Bukoba
MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini, Johnston Mutasingwa ameendelea kugusa maisha ya wananchi kwa vitendo baada ya kutoa msaada kwa makundi maalum pamoja na wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kata ya Kibeta katika kipindi iki cha Mfungo wa Kwalezima na Ramadhan
Msaada huo umekabidhiwa leo Machi 18,2026 kupitia Katibu wake Hamada Simba ambaye amesema Mbunge kwa sasa yupo nje ya jimbo akiendelea na majukumu ya ubunge lakini bado anawajali wananchi wake na kuhakikisha wanapata msaada wa mahitaji katika kipindi hiki Cha Mfungo
Amesema msaada huo unalenga kuwasaidia wananchi walio katika mazingira magumu, wakiwemo wazee, watu wenye ulemavu pamoja na kaya zenye kipato cha chini zinazofaidika na mpango wa TASAF.
Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na chakula sukari Sabuni na Vyakula mbalimbali vya kusaidia katika familia hizo katika Mfungo.
Kwa upande wao wananchi ambao wamenufaika na msaada huo wameonesha furaha na kutoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge wao, wakieleza kwamba hatua hiyo imewapa faraja kubwa na kuwasaidia kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutujali,Msaada huu umekuja wakati sahihi na utatusaidia sana katika maisha yetu,” amesema mmoja wa wanufaika.
Wakati huo huo Diwani wa Kata kibeta AnaStella Alphuns amesema kwa ujumla, tukio hilo limeendelea kuonesha mshikamano kati ya viongozi na wananchi pamoja na juhudi zinazoendelea za kuhakikisha ustawi wa jamii unaimarika, hasa kwa makundi yenye uhitaji zaidi.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...