VUNJO. 

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola amewapongeza walimu wa madrasa kwa juhudi zao za malezi ya kiroho na maadili kwa watoto na vijana kupitia elimu ya dini. 

Koola ametoa kauli hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kuhifadhi Qur'an yaliyofanyika mji wa mdogo wa Himo ambapo aliwapongeza washiriki wote kwa nidhamu, juhudi na kujituma katika mashindano hayo muhimu kwa ustawi wa jamii.

Mbunge aliwahimiza vijana kuendelea kushikamana na misingi ya imani, kuzingatia masomo yao darasani pamoja na kuepuka makundi yenye mienendo hatarishi ili kujenga jamii salama na Taifa lenye kizazi chenye maadili mema.

Katika kuhitimisha hafla hiyo, Koola alikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano, vyeti kwa washiriki wote, pamoja na zawadi maalum kwa walimu na majaji waliowezesha kufanikisha mashindano hayo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...