Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo rasmi wa biashara unaolenga kusimamia mazao yaliyokubaliwa na kuthibitishwa, kwa lengo la kuimarisha masoko na kipato cha wakulima.
Akizungumza Machi 30, 2026, katika kikao cha wadau wa mfumo huo kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, amesema mfumo huo unamruhusu mkulima kuuza mazao yake ghalani na kupata mikopo benki, pamoja na kuuza kwa bei yenye ushindani wa soko la dunia.
Ameeleza kuwa faida za mfumo huo ni pamoja na kuongeza tija, kurahisisha upatikanaji wa masoko ya mazao, pamoja na kuondoa upangaji holela wa bei kwani bei hufuata mwenendo wa soko la kimataifa.
Aidha, amesema mfumo huo unaimarisha uchumi wa wakulima kwa kuwapatia taarifa sahihi za bei na masoko, huku ukiongeza mapato ya serikali kupitia ushuru, kuboresha vipimo sahihi vya mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Amesema serikali imeanzisha mfumo huo ili kuondoa changamoto mbalimbali zikiwemo uuzaji wa mazao kabla ya mavuno, matumizi ya vipimo visivyo rasmi na mifumo kandamizi ya biashara, sambamba na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Mkuu wa Mkoa amewapongeza wadau mbalimbali wanaoshiriki katika utekelezaji wa mfumo huo, akiwemo WRRB, TMX, COPRA, DORECU pamoja na Tume ya Ushirika, kwa mchango wao katika kufanikisha mfumo huo mkoani Dodoma.
Ametoa wito kwa DORECU kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yao, kutoa elimu kwa wakulima na kuhamasisha uundwaji wa vyama vya msingi vya ushirika ili kuongeza kasi ya utekelezaji. Pia amesisitiza ujenzi wa maghala zaidi katika maeneo ya kimkakati, akibainisha kuwa hadi sasa maghala 39 tayari yamejengwa.
Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuajiri watumishi wenye weledi katika maghala hayo na kuhakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati ili waone matokeo chanya ya juhudi zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Dodoma (DORECU), Theresia Nyoka, amesema mkulima ni mhimili muhimu wa uchumi wa nchi na anapaswa kuheshimiwa. Ameiomba serikali kusaidia vyama vya ushirika kupata mitaji ili viweze kujiendesha kwa ufanisi.
Amesema DORECU imejipanga kuboresha huduma kwa kununua mizani ya kielektroniki 10 na kusambaza kompyuta kwenye vyama vya msingi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakulima.
Naye mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Aneth Mwangasa, amesema wizara inaendelea kufanya tathmini ya mfumo huo kila baada ya msimu wa kilimo na kutoa kipaumbele kwa mikoa mipya ikiwemo Dodoma, pamoja na kusaidia upatikanaji wa pembejeo kama mbegu na viuatilifu.
Katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji Mali, Aziza R. Mumba, amesema timu za wilaya zimejipanga kudhibiti usafirishaji haramu wa mazao na kusimamia sheria ndogo ili kuhakikisha mfumo unatekelezwa ipasavyo. Pia amebainisha kuwa ununuzi wa mazao kupitia madalali hautaruhusiwa.
Ametaja mikakati ya mwaka 2026 kuwa ni pamoja na kuhamasisha uzalishaji wa mazao yanayopitia kwenye mfumo, kuandaa na kuboresha maghala, kuimarisha vyama vya ushirika, kuhamasisha usajili wa waendesha maghala, kufanya tafiti na kuboresha miundombinu.
Amesema kuwa Vyama vya ushirika 14 vilitekeleza mfumo wa stakabadhi za ghala na kuuza jumla ya kilo 43,707,331 zikijumhisha ufuta kilo 19,300,802, Mbaazi kilo 24,092,900 na Dengu Kilo 313,629, na Halmashauri zilizofanya minada ya zao la mbaazi ni kondoa Mji, Kondoa, Chemba, Dodoma Jiji na Kongwa.
Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa miongoni mwa Mikoa, inayozalisha mazao ya ufuta, Mbaazi na dengu, ambayo mazao hayo yanauzwa kupitia mfumo wa masoko wa stakabadhi za ghala, na wadau katika utekelezaji wa mfumo huo ni wakulima, mamlaka za serikali za mitaa, vyama vya ushirika, watunza maghala, bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala, tume ya maendeleo ya ushirka, mamlaka ya udhibiti wa mazao mchanganyiko na soko la bidhaa Tanzania.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...