Na MWANDISHI WETU


NAIBU Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Ngeruko, amevitaka vituo vya kulea yatima nchini kuto kufuga watoto hao badala yake wawalee na kuwakuza katika maadili mema.

Ameyasema hayo Dar es Salaam katika futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Yono Auction Mart katika Kituo cha Kulea Yatima cha Mwana, kilichopo Vingunguti, juzi.

Akizungumza kwa niaba ya Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dk. Aboubakar Zubeir, Naibu Kadhi Sheikh Ngeruko, ameeleza vipo vituo vinavyo ishi na yatima kwa mfumo wa kuwafuga hali ambayo haiwakuzi katika njia inayo paswa.

“Yatima anatakiwa kulelewa siyo kufugwa. Alelewe kama mtata anaye lelewa akiwa nyumbani. Apewe mahitaji yote muhimu hususan elimu dunia na elimu ahera kulingana na imani ya mtoto,”alieleza Sheikh Ngeruko.

“Nataka tuandae semina itakayo washirikisha watu wanaoendesha vituo hivi vya kulea watoto. Tuwape elimu hii ya kuto kuwa fuga badala yake wawalee ili baada ya kukua wajitegemee kimaisha na kuwa na maadili mema,”alisema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Yono Auction Mart, Stanley Kevela, alisema wataendeleza utamaduni wa kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu hususan kutoa sadaka kwa yatima kwani hata vitabu vitakatifu vimeelekeza hilo.

Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Yono Auction Mart, Dk.Scolastica Kevela, alikemea vikali wanawake wanao tupa watoto baada ya kujifungua na kuitaka jamii kulaani vitendo hivyo.

Dk. Scolastica ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Njombe, alimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kitendo cha kishujaa cha kumwasili mtoto mchanga hivi karibuni.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia kwa kitendo hicho kinacho thibitisha, upendo na kujali malezi ya watoto. Nikiwa mmoja wa wanawake wanao kemea ukatili na toa wito kwa jamii kusimamia malezi ya watoto wetu,”alisema.

Alieleza,kampuni yake itaendelea na utamaduni wa kutoa gawio kwa jamii hususan wenye mahitaji maalumu, kushiriki shughuli za maendeleo kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia.

“Wito wangu kwa jamii. Kama umeajaaliwa kipato toa kiasi kwa jamii hasa watoto hawa wenye mahitaji maalumu. Mungu atakubariki kwani mali na fedha vyote tutaviacha hapa duniani,”alisema Dk. Kevela.

Uongozi wa Kituo cha Mwana ulishukuru wadau hao kuwakumbuka watoto katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuomba jamii kuendelea kusaidia kituo hicho chenye watoto 55 wa jinsia na rika mbalimbali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...