Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ametembelea Bandari ya Durban iliyopo nchini Afrika Kusini, kwaajili ya kujionea utendaji na uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo inayohesabika miongoni mwa bandari kuu za kontena barani Afrika.
Bandari ya Durban ina jumla ya gati 58 zinazohudumia aina mbalimbali za mizigo ikiwemo makasha (containers), magari, mizigo ya kawaida (break bulk), mizigo mikavu (dry bulk), pamoja na abiria. Kwa mwaka, bandari hiyo hushughulikia makasha milioni 2.6, tani milioni 13 za mizigo mikavu, tani milioni 4.6 za break bulk, magari 560,000 na takribani kilolita milioni 22 za mizigo ya vimiminika (liquid bulk).
Akizungumza baada ya ziara hiyo iliyofanyika Machi 20, 2026, Waziri Kihenzile amesema ameridhishwa na kiwango kikubwa cha uwekezaji katika miundombinu ya bandari na reli, pamoja na namna ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi unavyoongeza ufanisi wa huduma bandarini.
Ametolea mfano mkataba wa miaka 25 kati ya bandari hiyo na kampuni ya ICTSI ulioanza Januari 2026 kwa ajili ya kuendesha Pier 2, unaolenga kuongeza uwezo wa kuhudumia makasha (TEUs) na kuongeza kasi ya utendaji kazi bandarini kwa zaidi ya mara mbili.
Waziri huyo amesema uzoefu huo unaonesha umuhimu wa sekta binafsi katika kuboresha ufanisi wa bandari, ambapo amebainisha kuwa Tanzania tayari inanufaika na ushiriki wa sekta binafsi kupitia kampuni kama DP World na Adani Ports (kupitia TEAGTL/TICTS) katika uendeshaji wa sehemu ya bandari.
Aidha, ameeleza kuwa juhudi hizo zinaenda sambamba na uwekezaji wa Serikali katika miundombinu ya reli, ikiwemo Standard Gauge Railway (SGR), Meter Gauge Railway (MGR) na TAZARA, ili kuharakisha upakiaji, upakuaji na usafirishaji wa mizigo.
Amehitimisha kwa kusema kuwa Bandari ya Dar es Salaam inaendelea kuimarika kila siku na kuwa lango lenye ushindani mkubwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, huku ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ukiendelea kuleta matokeo chanya katika sekta ya uchukuzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...