Na Janeth Raphael - MichuziTv
Rais Samia amesema Taifa litamkumbuka William Lukuvi kama kiongozi aliyegusa maisha ya wengi kwa moyo wake wa upendo, hekima, na kujitolea kwa dhati katika utumishi wa umma.
"Hayati Lukuvi atabaki katika kumbukumbu zetu si tu kwa nafasi alizoshika, bali kwa namna alivyoweza kujenga mahusiano mema na ya kudumu ndani ya jamii"
Pia Rais Samia amesema LUKUVI alikuwa kiongozi aliyesikiliza, aliyeshirikiana na makundi mbalimbali, na aliyethamini mchango wa kila mmoja katika kujenga taifa.
Katika kipindi hicho ambacho dunia inakumbwa na changamoto nyingi na mabadiliko yasiyotabirika, umuhimu wa kuwa na viongozi wenye uzoefu mpana na waliopitia ngazi mbalimbali za uongozi hauwezi kupuuzwa
"Tulimuhitaji sana ndugu Lukuvi leo—zaidi hata kuliko jana—ili kuendelea kutoa mwongozo na busara katika nyakati hizi ngumu"
Aida Rais Samia amesema Maisha na utumishi wa LUKUVI vinatufundisha somo muhimu sana: kwamba uongozi ni dhamana, si fursa ya kujinufaisha, n wajibu wa kuitumikia jamii kwa uaminifu, uwajibikaji, na moyo wa kujitolea bila kuchoka, Haya ndiyo maadili aliyoyaishi, na huu ndio urithi wake kwa taifa letu"
Hata hivyo Rais Samia amesema ni jukumu letu sasa kuuenzi na kuuendeleza urithi huo Tuige mfano wake kwa kuimarisha mshikamano, kuheshimiana, na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya wote, kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumemuenzi kwa vitendo, na kuhakikisha kuwa mchango wake unaendelea kuzaa matunda kwa vizazi vijavyo.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...