Mamlaka za maji na usafi wa mazingira za Moshi, Nzega na Biharamulo zimetwaa tuzo za mamlaka bora nchini, katika tathmini ya ripoti ya EWURA ya utendaji wa mamlaka za maji iliyozinduliwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb) leo tarehe 19 Machi 2026, mjini Morogoro.

Aidha, mamlaka 27 zilitambuliwa kwa kuwasilisha kwa asilimia 100 tozo ya udhibiti.

Taarifa ya hiyo ya Tathmini imepima Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 83 zinazotoa huduma katika mikoa, wilaya na miji midogo , katika hafla iliyofanyika mjini Morogoro.

Waziri Aweso ameipongeza EWURA kwa kuandaa taarifa hiyo muhimu iliyobainisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira nchini.

Kwa mujibu wa EWURA, tathmini hiyo imeonesha mafanikio katika ongezeko la uzalishaji wa maji kwa 19.3%, wateja kufikia milioni 1.8 na mapato kuongezeka kwa 14%. Hata hivyo, changamoto kama upotevu wa maji (42.3%) na uhaba wa miundombinu ya majitaka bado zinaendelea.

Mhe. Aweso amezitaka mamlaka za maji kuendelea kuboresha huduma kwa kuzingatia ubora, uwazi na uendelevu.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...