Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeeleza kuwa hali ya upatikanaji wa mafuta nchini bado ni shwari, huku bei zikiwa himilivu, ambapo mafuta yaliyopo yanatosheleza kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na uhaba wa mafuta duniani uliotokana na vita inayoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Dkt. Mataragio amesema:
“Mafuta yaliyopo nchini kwenye matenki, Petrol tuna lita 95,256,342; mafuta ya petrol yaliyowasili nchini ni lita 1,466,337; mafuta yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 138,737,332. Hivyo, jumla ya mafuta ya Petrol yatakayokuwepo ni lita 380,677,011, na yanatosha kwa matumizi ya siku 61.”
Ameongeza kuwa kuna mikataba ya mafuta iliyoingiwa na mzabuni yenye jumla ya lita 183,500,450 ambayo yatafika nchini mwezi wa nne, hivyo jumla ya mafuta ya Petrol yaliyopo kwenye matenki, yatakayowasili nchini kwa meli pamoja na yaliyopo kwenye mikataba ni lita 563,682,461, kiasi ambacho kinatosheleza kwa siku 91.
Kwa upande wa mafuta ya Diesel, amesema mafuta yaliyopo kwenye matenki ni lita 55,744,397; yaliyowasili nchini ni lita 122,893,285; na yaliyopo njiani kwenye meli ni lita 184,662,480. Hivyo, jumla ya mafuta ya Diesel ni lita 362,433,845, yanayotosha kwa matumizi ya siku 44.
Amefafanua kuwa mafuta ya Diesel yaliyopo kwenye mikataba na wabuni ni lita 167,321,343. Kwa ujumla, mafuta yaliyopo nchini, yanayokuja kwa meli na yaliyopo kwenye mikataba ni lita 530,621,505, kiasi kitakachotosheleza kwa siku 64.
Kwa upande wa mafuta ya ndege, Dkt. Mataragio amesema yapo ya kutosha ambapo yaliyopo kwenye matenki ni lita 35,241,028 na yaliyopo kwenye mikataba ni lita 23,779,725. Jumla yake ni lita 59,020,753, zitakazotosheleza kwa siku 97.
Ameeleza kuwa kutokana na hali ya vita kuendelea, kunatarajiwa ongezeko la bei za mafuta kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...