Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe ameziagiza halmashauri zote kwenye mikoa ya Geita, Tabora na Iringa kuendelea kutenga kiasi cha sh 1,000 kwenye bajeti zao kwa kila mtoto wa chini ya miaka mitano ili kuboresha miradi ya lishe katika halmashauri hizo.

Ametoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuimarisha Huduma za Lishe katika mikoa ya Geita, Iringa na Tabora ili kusaidia kupunguza changamoto za udumavu, ukondefu na utapiamulo wa watoto.

Profesa Shemdoe ameitaka mikoa ya Geita, Iringa na Tabora kuimarisha ufuatiliaji wa mradi jumuishi wa lishe na shughuli zote zinazotekelezwa katika jamii kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya lishe

Mradi wa Kuimarisha Huduma za Lishe  unatekelezwa chini ya ufadhili wa taasisi ya BWP ya nchini Uingereza kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 2 malengo makuu yakiwa ni kuimarisha lishe na maendeleo ya watoto.

Halmashuri zote zimetakiwa kuhakikisha zinatoa takwimu sahihi na kwa wakati ili kuzingatia utoaji huduma sahihi kwa kuzingatia ushahidi unaotokana na takwimu.

Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Profesa Tumaini Nagu amesema kuwa kupitia  mradi huu serikali itaongeza kasi ya ufuatiliaji wa huduma bora za malezi na makuzi ya awali ya mtoto hususani katika vituo ya kulelea watoto mchana,

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Luitfrid Nnally amesema kuwa pamoja na nchi kuwa na kiwango kikubwa cha vyakula lakini bado watoto wanapata utapiamlo katika mikoa hii mitatatu kutokana na kukosa matunzo kutokana na shughuli nyingi za wazazi hususani kilimo

Mwakilishi wa taasisi ya BWP, Dr Taye Balcha alisisitiza kuwa mradi huo umezingatia tathimini ya serikali na hivo na kutambua kuwa wahanga wakubwa wa udumavu ni watoto.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigella aliahidi kuwa mkoa wa Geita kwa kushirikiana na mikoa inayonufaika na mradi huo watatumia fursa hiyo kupunguza kiwango cha lishe kilichopo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...